July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Mwanri: Naomba radhi

Agrey Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Tabora

Spread the love

AGREY Mwanri, Mkuu wa Mkoa wa Tabora ameomba radhi kufuatia kauli yake aliyoitoa mwanzoni mwa mwezi Aprili 2019 kwamba, Mungu amshukuru Rais John Magufuli kutokana na kazi anazofanya za kuliletea maendeleo taifa. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akizungumza na wanahabari mkoani Tabora, Mwanri amesema, hakuna binadamu anayeweza kuchukua nafasi ya Mungu huku akisistiza kwamba, atakua amechuja sana endapo ataamini hilo.

Mwanri amefafanua kuwa, kauli yake haikuwa na maana mbaya bali ilitafsiriwa tofauti na baadhi ya watu.

Amesema, dhamira yake ilikua ni kutaka kuona kwamba Mwenyezi Mungu anamshukuru Rais Magufuli kutokana na mema anayofanya ya kutetea masilahi ya wangine.

“Ila nilichojifunza ni kwamba, inapopelekwa habari inapokelewa na masikio mengi usifikiri hata kama uko sawa itapokelewa hivyo hivyo, bali itapokelewa tofauti.

“Sina cha zaidi ya kuomba msamaha kwa sababu nimeshafafanua na mimi walioninukuu vibaya natangaza kuwasemehe,” amesema Mwanri.

error: Content is protected !!