April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Kabati: Mchungaji Msigwa ana bahati

Spread the love

RITA Kabati, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoani Iringa amesema, mambo mengi anayozungumza Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, yanatekelezwa na serikali. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kuhusu maendeleo ya jimbo hilo analotoka Kabati amesema, Serikali ya CCM imekuwa ikifanyia kazi hivyo jimbo hilo kupiga hatua.

“Mimi naingia Jimbo la Iringa Mjini ambalo mbunge wangu wa jimbo ni Mchungaji Msigwa, ana bahati kwasababu vitu vingi sana nimekuwa nikivisema na vimefanyiwa kazi na Serikali ya Chama cha Mapinduzi,” amesema.

Kabati amesema, walipoingia bungeni kulikuwa na tatizo la msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Iringa, ambapo alisimamia hoja ya upatikanaji wa Hospitali ya Wilaya ambapo iimepatikana.

“Naweza kusema, nimechangia sana kuwepo Hospitali ya Wilaya kwasababu, niliisemea na kuhakikisha inasajiliwa na inaanza kufanya kazi na mpaka leo, bado naisemea iweze kulaza hata wagonjwa,” amesema.

Hata hivyo Kabati  amesema, amepambana kuhakikisha wanahuisha Msitu wa Kihesa ambao ulikuwa chini ya halmashauri ili kutumia viwanja vya msitu huo kwa utalii.

“Kitovu cha Utalii Nyanda za juu Kusini kipo Iringa na tushukuru kwamba, hata uwanja wa ndege safari hii Bombardier itatua kwasababu tuliipigania sana,” amesema.

Amesema kuwa, kutoka na juhudi zake anazozifanya, amelisemea suala la machinjio ambayo imekuwa haipatiwi pesa kwa ajili ya kuyaendeleza hivyo mwaka huu, wamepatiwa Sh. 1.1 Bilioni  kwa ajili ya kuyaendeleza na kuwa chanzo kikubwa cha mapato na ajira katika mkoa huo.

https://youtu.be/KXCuA54fUpQ

error: Content is protected !!