November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC K’njaro ataka ‘spidi’ ujenzi wa madarasa

Anna Mghwira, Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro

Spread the love

ANNA Mghwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ameagiza watendaji na wakurugenzi wa mkoa huo kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madarasa mapema ili wanafunzi waliochaguliwa kuanza Kidato cha Kwanza, wasikose nafasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro…(endelea).

Ametoa kauli hiyo kwenye kikao maalum cha kujadili changamoto ya uhaba wa madarasa na kwamba, katika wilaya za Hai, Moshi Vijijini, Siha na Same wanakabiliwa na uhaba wa madarasa yapatayo 60.

“Wanafunzi 2,900 hawataweza kuendelea na masomo ya Kidato cha Kwanza ambapo Hai wataishindwa kuendelea ni 890, Moshi Vijijini 350, Same 1,414 na Siha 305,” amesema Mghwira.

Pia amemtaka Ofisa Elimu wa Mkoa, Paulina Mkwama kuhakikisha anarekebisha Ikama ya Walimu katika baadhi ya wilaya kutoka na upungufu mkubwa wa walimu unaokabili mkoa huo.

error: Content is protected !!