MKUU wa mkoa wa Songwe Dk. Fransis Michael amewapa onyo maafisa kilimo wa wilaya zote mkoani humo kuacha kukaa maofisini na badala yake waende vijijini kuwapa ushauri wa kitaalam wakulima. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).
Dk. Michael aliyasema hayo leo tare he 14 Novemba, 2023 wakati wa kikao cha wadau wa kilimo kilichofanyika kwenye ukumbi ulipo kwenye ofisi za mkoa huo.
Alisema yeye kama mkuu wa mkoa amekuwa akifanya ziara za kikazi vijijini kila wakati huku akiwashangaa maafisa hao kukaa maofisini licha ya serikali kuwapa pikipiki na mafunzo ya mara kwa mara.
“Mmepewa usafiri wa pikipiki na Rais Dk. Samia muwatembelee wakulima lakini ninyi hamfanyi hivyo, mnakwenda nazo kwenye mabaa, katibu tawala shughurika na watumishi hawa waende vijijini.” amesema Dk. Michael.
Ameongeza kuwa vijiiini wakulima wengine hawajuhi mbolea watazipataje, badala wapate ufafanuzi na msaada kwa maafisa kilimo lakini hawaonekani kwa wakulima, na kwamba anapokuwa vijijini anazipata taarifa zote.
Katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda aliyapokea magizo hayo huku akiruhusu wadau wa kilimo kutoa changamoto zinazohusu kilimo ambapo malalakiko yaliyotolewa ni maafisa hao kutofika vijijini na kupanda bei ya mbegu za mahindi.
Leave a comment