Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aweka shada kaburi la Dk. Kaunda
Habari za Siasa

Rais Samia aweka shada kaburi la Dk. Kaunda

Spread the love

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa uhuru wa Zambia.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rais Samia ameweka shada hilo ikiwa ni ishara ya kutoa heshima na kutambua  walioongoza harakati za kuliltea uhuru Taifa hilo mwaka 1964.

Baada ya kuweka shada kwa mashujaa, Rais Samia pia ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda jijini Lusaka.

Leo Zambia inaadhimisha miaka 59 tangu ipate Uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1964 na tukio la kuweka shada hufanywa kila mwaka wakati wa maadhimisho haya.

Rais Samia amealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru litakalofanyika baadaye leo kwenye Ikulu ya Zambia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!