RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Septemba 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia amemteua Balozi Kingu, baada ya kuivunja Bodi ya REA.
“Rais Samia amevunja Bodi ya REA na amemteua Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi REA,” imesema taarifa ya Yunus.
Katika hatua nyingine, Rais Samia amemteua Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), John Ulanga, kuwa balozi.
Leave a comment