January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia atangaza kufanya mabadiliko mawaziri, makatibu wakuu…

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ameutangazia umma wa Watanzania kuwa hivi karibuni atafanya mabadiliko ya nafasi za viongozi mbalimbali wa Serikali anayoiongoza kuanzia mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi na wakuu wa mikoa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Januari, 2022 wakati akipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa awali wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.

Mpango huo ambao uliozinduliwa Oktoba mwaka jana, unatekelezwa kwa fedha za mkopo wa Sh. trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa kunufaisha sekta ya elimu, afya, maji, maliasili na utalii.

Aidha, akizungumzia kelele za wanaodai Serikali yake inakopakopa, amesisitiza hizo ni homa ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hivyo atawaweka pembeni ili wakutane mbele ya safari.

“Nataka niwaambie nitatoa list mpya karibuni, wale wote ninaohisi wanaweza kwenda na mimi kwenye kazi ya maendeleo ya Watanzania, nitakwenda nao.

“Lakini wote ninaohisi ndoto zao ni kule na wanafanya kazi kwa ajili ya kule nitawapa nafasi waende wakajitayarishe vizuri huko nje, kwa sababu nikiwatuma ndani nitawasumbua kwa hiyo bora niwape nafasi wakajitayarishe tukutane huko mbele ya safari,” amesema.

Amesema lengo la Serikali ni maendeleo kwa watanzania hivyo viongozi anaowateua wanatakiwa kwenda kuleta maendeleo.

“Uongozi huletwa na Mungu aliyepangiwa ndiye atakayekaa,” amesema.

Amewaonya wakuu wa mikoa kuwa amewateua ili wamsaidie.

“Wakuu wa mikoa nimekuwekeni nikiamini kule nilikowakasimia madaraka mtakwenda kusimamia kazi na wengine wote kama vile makatibu wakuu na mawaziri.

“Nimekaa nadhani huu ni mwezi wangu wa nane sijui! nilisema nilikuwa nawasoma nanyi mnanisoma na siku nimefanya mageuzi kidogo ya mawaziri nikasema hapa nimeweka koma kazi inaendelea,” amesema.

error: Content is protected !!