Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ‘amlipua’ Spika Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ‘amlipua’ Spika Ndugai

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewapongeza wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusimama kutetea mkopo wa Sh.1.3 trilioni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkopo huo usiokuwa na riba ni kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) wenye lengo la kuchochea mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Leo Jumanne, tarehe 4 Januari 2022, Rais Samia amepokea taarifa ya utekelezaji wa fedha hizo kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu, afya, maji na miundombinu, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Amewapongeza viongozi mbalimbali wa Serikali na chama chake- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusimamia vyema fedha hizo na kuwajibu waliojitokeza kuhoji mikopo hiyo.

“Niwashukuru mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya kwa kusimamia miradi hii lakini niwashukuru zaidi na zaidi wenyeviti wa CCM kwa kusimama na kutetea mkopo huu ulioleta maendeleo. Walijotokeza kuhoji mkopo mlisimama na kusema,” amesema Rais Samia.

Viongozi hao wa CCM kama mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Singida na Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) walijotokeza kumjibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Walimjibu baada ya Spika Ndugai kukosoa mkopo huo wa Sh.1.3 trilioni na kusema, bora kujibana kwa kutumia fedha za ndani kama tozo kugharamikia miradi ya maendeleo.

Spika Ndugai alikwenda mbele zaidi na kudai, iwapo madeni yatakuwa makubwa, yanawezekana nchi ikapigwa mnada.

Kauli hiyo ilimuibua Rais Samia na kusema serikali anayoingoza, itaendelea kukopa huku wenyeviti wa CCM wakimshambulia kama nyuki, Spika Ndugai wakimtaka kutomkwamisha Rais Samia.

Baada ya kushambuliwa vilivyo, jana Jumatatu tarehe 3 Januari 2022, Spika Ndugai alijitokeza kumwomba radhi Rais Samia na wananchi kwa kauli hiyo aliyoitoa.

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Amesema, ameshangazwa na kiongozi huyo kusimama mbele za hadhara kukosoa mkopo huo wakati bajeti na taarifa mbalimbali zinapitia kwenye bunge lake, “na hiyo ni homa yam waka 2025.”

Rais Samia amesema, “nilipotishwa huu mzigo, kuna mtu alikuja akanipa pole na hongera na akasema atakayekusumbua kwenye kazi hii ni mwenye shati la kijani mwenzako si wa upinzani na hili ni wanaoitizama 2025.”

Akizungumza kwa sauti ya chini Rais Samia amesema, “kelele za wanaopiga kelele hawanisumbui ila na mimi nina moyo wangu si wa glasi ni wa nyama ulioumbwa na Mungu, nishikeni mkono twende sote.”

2 Comments

  • Asante mama shaka ondoa tupo pamoja nia na madhumuni yako ni kujenga taifa letu wasio kutakia mema maana yake hawalitaki mema taifa la tanzania lakini wache waseme ovyo mwisho watachoka taifa letu linazidi kuendelea kwa vitendo asante mama kazi iedelee uhuru na umoja kazi ya ccm

  • Kaza Moyo mama acha wapige kelele ww fanya maendeleo,madarasa tumeyaona,maji yapo,vituo vya afya vinaonekana,n.k ipo siku lindugai litakiri kwa kinywa chake.bora mh.ssh unatuambia unapokopa awamu ya 5 pesa zilikopwa matrilioni na hatukupewa taarifa tunaambiwa ni makusanyo ya ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!