Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia afichua simu ya waziri ilivyomnyima usingizi
Habari za Siasa

Rais Samia afichua simu ya waziri ilivyomnyima usingizi

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na ‘stress’ za madeni ya nchi siku moja Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. Mwigulu Nchemba alimpigia simu mara tatu usiku bila kujali kuwa amelala. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amefichua hayo leo tarehe 4 Januari, 2022 wakati akipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa awali wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.

Mpango huo ambao ulizinduliwa Oktoba mwaka jana, unatekelezwa kwa fedha za mkopo wa Sh trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa kunufaisha sekta ya elimu, afya, maji, maliasili na utalii.

Huku akitumia msamiati wa ‘debt distress’, uliotumiwa na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango katika hotuba yake leo, Rais Samia amesema Dk. Mwigulu naye alikuwa amechanganyikiwa kutokana na madeni hayo.

Rais Samia amefunguka kuwa alipopokea simu ya Mwigulu na kusabahiana usiku huo, waziri huyo alimweleza kuwa IMF wamempigia kumweleza kuwa na zile zilizobaki wataipatia Serikali kwa vigezo vya bila riba kwa miaka 20.

“Nikawambia habari nzuri… mbona uko juujuu, Akaniambia tuna madeni ambayo yamesha- mature (yameshaiva). Interest rate (riba) ni kubwa tutakwenda kufanya kazi ya kukusanya tulipe madeni. Hakuna maendeleo.

“Nikamwambia Mwigulu hebu usinikate usingizi wangu, njoo kesho tukae tuzungumze, siku ya pili akaja na listi yake ya madeni yalivyoiva na nini, nami na Katibu Mkuu Kiongozi tukaka naye, akatupitishaaa!

“Nikamuuliza sasa unasemaje, akasema sasa huu mkopo tuliopata bila riba, nusu tuingize huko, tushushe stress za deni angalau tupate muda tuvute pumzi, tukikusanya huko mwaka unaofuata tutakenda kulipa lakini hapa tuziingize hizi. Tukatizamana machoni tukasema eeh akili, kwa hiyo tukakubaliana,” amesimulia.

Amesema awali walikuwa wameshaanza kuchanganyikiwa na mikopo hiyo lakini sasa wametumia mkopo huohuo kushusha ‘stress’

“Mambo ni kwa akili, unakopa kusiko riba. Jamani hata kwenye maisha yetu si ndio tunavyofanya? Unakuwa na mikopo huku imekukaa hapa shingoni, unakwenda benki nyingine unakopa, unalipa mkopo ambao umeshatimia unaanza mkopo mpya. Uongo?

“Kwa nchi kuna tatizo gani tukifanya hivyo?, tutakopa mikopo isiyoriba tulipe ile ya riba kubwa ili tupate nafuu, hiyo ndio debt distress, kwa hiyo tunafanya distressing ya deni,” amesisitiza na kuongeza kuwa “Tunapunguza uchovu wa deni, kwa hiyo mwalimu wetu yupo hapa (Dk. Mpango) atatusaidia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!