Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Rais Samia ataja kazi tatu Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, ‘viongozi wanayumbayumba kuleta maendeleo’
Habari

Rais Samia ataja kazi tatu Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, ‘viongozi wanayumbayumba kuleta maendeleo’

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema uanzishwaji wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere itakwenda kujibu kasoro zilizokuwa zimejitokeza katika uongozi wa vyama vya ukombozi Kusini mwa Bara la Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Pia amesema chuo hicho cha kimkakati kitaimarisha vijana na makada ambao watakwenda kufanya kazi katika vyama hivyo vya siasa na serikali za nchi husika. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Vyama hivyo vya ukombozi ambavyo vimeshirikiana kujenga chuo hicho kwa ufadhili wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ni Chama Cha Mapinduzi – CCM (Tanzania), Frelimo (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ANC (Afrika Kusini), ZANU-PF (Zimbabwe) na NPLA (Angola).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Februari, 2022 wakati akifungua Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Akinukuu baadhi ya maandiko ya wasomi waliojenga hoja kukosoa udhaifu wa uongozi wa vyama hivyo vya ukombozi, Rais Samia amesema maandiko hayo yalikuwa yanawabadilisha vijana kimtizamo na kimawazo.

“Nimepitia maandiko kadhaa ya watalaamu walioandika na moja limeandikwa hivi, ‘Can former liberty lead in to the future?’, maana yake ni kwamba wale wakombozi wetu wataweza kuiongoza Afrika kuendelea mbele kwenye maendeleo zaidi.

Amesema andiko hilo kwa kiasi kikubwa limesema viongozi wa Afrika kutoka vyama vya ukombozi hawatoweza kuisaidia bara hilo kupiga hatua kimaendeleo.

“Linabadilisha akili na mtazamo wa vijana wetu wa Afrika, kwamba viongozi wetu huko nyuma wasingeweza kupeleka nchi zetu mbele kwenye maendeleo.

“Sasa kuwepo kwa chuo hiki kitarekebisha hilo na kuweka mawazo mtazamo wa vijana wetu kule tunapotaka waelekee,” amesema.

Amenukuu andiko lingine kuwa ni ‘Freedom fighter believe the right to govern but struggle to deliver the economic development that Africa needs.

“Kwamba viongozi wetu wanang’ang’ania kukaa madarakani lakini wanayumbayumba kuleta maendeleo ya kiuchumi ya Afrika,” amesema.

Amesema andiko hilo pia linabadilisha mtazamo wa vijana dhidi ya maendeleo ya nchi za Afrika.

“Sasa chuo hiki kitawaweka pamoja vijana na watu wetu ambao watafanya kazi kwenye serikali zetu na vyama vyetu na kuonesha mifano halisi ambayo nchi zetu zinafanya kuletea maendeleo kwa nchi zetu… itakwenda kubadilisha mtazamo na mawazo ya watu wetu.

“Pia nimesoma andiko ambalo lilikuwa linasifia sana nchi ambazo vyama vya ukombozi vimetolewa madarakani.

“Na hili andiko linawahimiza vijana kujiunga na vyama vya kimageuzi ambayo wanatakiwa kugeuza nchi zao ili kutoa vyama vilivyokomboa mataifa haya ya Bara la Afrika,” amesema.

Ameongeza kuwa uwepo wa chuo hicho utakwenda kujibu yote hayo ambayo yameandikwa miaka mingi.

“Lakini kitakwenda kujibu kwa kutoa mafunzo kwa vijana wetu, makada wetu watakaokwenda kufanya kazi kwenye vyama na serikali zetu,” amesema.

Pia amesema chuo hicho kitakwenda kufanya kazi ya kufanya tathmini ya maendeleo kwenye nchi Afrika kupitia Umoja wa Afrika ambao umeweka mpango unaitwa ‘APRM’.

“Kwa hiyo chuo hiki kitakwenda kuigiza kama APRM na kufanya tathmini ya maendeleo tuliyopata kwa nchi zetu sita lakini pia kuangalia mbele tuna mtazamo gani na vipi tutakwenda kwa kupitia chuyo hiki,” amesema.

Mbali na kupongeza wazo la waasisi (marais) ambao waliwaza kujenga chuo pia ametoa wito kwa wale watakaopewa jukumu la kukisimamia, kukitunza ili kiendelea kutoa huduma stahiki kwa Waafrika.

Amesema kupitia chuo hicho, viongozi, makada wa vyama vya mataifa hayo sita na watendaji wa taasisi za kimkakati watapatiwa mafunzo ya muda mrefu, kati na mfupi.

“Kwa mfano kuna wakuu wa mikoa na taasisi wametoka hapa,” amesema.

Amesema mafunzo yatakayofundishwa yatahusu masuala ya uongozi na itikadi ambayo ni miongoni mwa matatizo makubwa yanayozikabili nchi za Afrika katika zama hizi za demokrasia ya vyama vingi.

“Nilikuwa kwenye nchi moja za ukombozi, tulikuwa tunazungumza na vijana na kuwaambia jinsi viongozi wao walivyokomboa nchi zao, walitujibu kwamba ‘walishafanya upande wao sasa je!, ni zamu yetu watuache na sisi tufanye ya kwetu’. Hawa ndio vijana wanaojaribu kujengwa na maandiko mbalimbali.

“Niombe chuo hiki kifanye kazi tuliyokusudia ya kubadili maono ya vijana wetu na kuwajenga vile tunavyotaka,” amesema.

Aidha, amesema amefurahi kukamilika kwa wazo la ujenzi wa chuo hicho kwani uhai wa vyama vya na mataifa hayo kupitia vyama sita la tarehe 8 Juni, 2012 leo limetimia.

Amesema katika chuo hicho cha kimkakati kilianza kwa kutoa mafunzo ya majaribio yaliyoanza wiki mbili zilizopita lakini mafunzo kamili yataanza mwezi ujao na kushirikisha vyama vyote.

Aidha, mbali na kushukuru makatibu wakuu wa vyama hivyo waliopendekeza jina la Mwalimu Nyerere, pia amewaomba viongozi hao kuleta makada na watu mbalimbali kuja kusomea uongozi katika chuo hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

HabariHabari Mchanganyiko

Mwili wa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine wawasili, kuzikwa Mbeya

Spread the loveMWILI wa Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, aliyefia...

error: Content is protected !!