January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia apangua mawaziri 9, manaibu 3

Ummy Mwalimu

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Januari, 2022 amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu huku akiwabadilisha wizara mawaziri tisa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa iliyosomwa kwa umma kupitia vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga, Rais Samia amembadilisha Jenista Mhagama ambaye alikuwa Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Uratibu na Bunge kueleke Ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi na Utawala bora.

Amemhamisha Ummy Mwalimu ambaye alikuwa Ofisi ya Rais Tamisemi kwenda wazara ya aFya, George Simbachawene ametoka wizara ya mambo ya ndani kwenda wizara ya katiba na sheria

Profesa Joyce Ndalichako ametoka wizara ya elimu, sayasi na Tekonolojia kwenda kuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu.

Rais Samia amemhamisha Innocent Bashungwa kutoka wizara ya utamaduni, sanaa na michezo na sasa atahamia ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) huku Prof. Adolf Mkenda ambaye alikuwa waziri wa kilimo ameelekea wizara ya elimu, sayansi na teknolojia.

Dk. Dorothy Gwajima ambaye alikuwa wizara ya afya sasa atakwenda wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na wenye mahitaji maalum wakati Mohamed Omar Mchengerwa ambaye alikuwa ofisi ya rais menejimenti, utumishi na utawala bora amehamia waziri ya umataduni, sanaa na michezo.

Rais Samia pia amemhamisha Dk. Ashatu Kijaji ambaye alikuwa waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari kuwa waziri wa uwekezaji, viwanda na biashara.

Aidha, Rais Samia pia amewahamisha manaibu mawaziri watatu ambapo Khamisi Khamisi ambaye alikuwa wizara ya mambo ya ndani amehamishiwa ofisi ya makamu wa rais muungano na mazingira.

Hamad Chade ambaye alikuwa ofisi ya makamu wa rais amehamishiwa wizara ya fedha na mipango wakati Mwanaidi Hamisi ambaye alikuwa wizara ya afya na maendeleo ya jamii atakuwa naibu waziri wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu.

error: Content is protected !!