January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua Manaibu mawaziri watano, Mavunde arudi, Ridhiwani Kikwete apenya

Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Januari, 2022 amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu huku akiteua manaibu mawaziri wapya watano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa iliyosomwa kwa umma kupitia vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga, Rais Samia amemteua Athony Mavunde kuwa Naibu Waziri wa Kilimo,

Amemteua Jumanne Abdalah Sagini kuwa naibu waziri mambo ya ndani wakati Dk. Lemomo Ole Kiruswa ameteuliwa kuwa naibu waziri wizara ya madini,

Pia Ridhiwani Kikwete ameteuliwa kuwa naibu waziri wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi wakati Atupele Mwakibete ameteuliwa kuwa naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi upande wa sekta ya uchukuzi.

error: Content is protected !!