RAIS Samia Suluhu Hassan leo tarehe 8 Januari, 2022 amefanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri na nafasi za makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu huku akiwatema mawaziri watano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa iliyosomwa kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga imeonesha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ametemwa na nafasi yake imechukuliwa na George Simbachawene.
Katika mabadiliko hayo pia Rais Samia amemuweka kando aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ambaye nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Naibu wake, Dk. Angelina Mabula.
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo pamoja na Waziri wa Uwekezaji, Geofrey Mwambe wote wameachwa katika mabadiliko hayo ambayo yameunganisha wizara hizo mbili kuwa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji huku waziri wake akiteuliwa kuwa Dk. Ashatu Kijaji.
Pia Rais Samia amemtema Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo.
Wengine ni Naibu Waziri wa Madini, Prof Shukrani Manya ambaye nafasi yake imechukuliwa na Dk. Lemomo Ole Kiruswa.
Kazi kwako hakuna wakukupangia jiachie utakavyo.
Kwa nini hawa walioachwa wote wababa. Siungechanganya ili iwe 50 kwa 50.
Mabadiliko ni jambo la kawaida duniani na wala sio shall kuna mabadiliko ya hali ya hewa kuna usiku na mchana. Katika soccer kuna dk 90.wachezaji 22.katika hao 22.cocha anao uwezo wa kufanya mabadiliko wako wachezaji atawatoa and kuwaigiza wengine kwa ushauri au hata bira ya ushauri mabadiliko maana yake ni maendeleo