Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aonya viongozi wanaosubiri maelekezo kutoka juu
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia aonya viongozi wanaosubiri maelekezo kutoka juu

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan leo jumapili amewaonya viongozi wa umma kuacha ‘kujidogosha’ kwa kutekeleza majukumu yao kwa kusubiri maelekezo kutoka juu badala yake wawe wabunifu na kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, miongozo, sheria na mipango ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea.)

Kauli hiyo ya Rais imekuja baada ya viongozi wengi wa umma kuogopa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi katika utekelezaji wa majukumu yao na kubaki kusubiri maagizo kutoka juu.

Rais Samia maagizo hayo  leo tarehe 27 Agosti 2023 wakati akifunga mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, yaliyofanyika katika Taasisi ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani.

Amesema katika uongozi wake hatashusha maelekezo kwa viongozi hao kuhusu nini wanapaswa kufanya, badala yake anataka kuwaona wanakuwa na ndoto kulingana na mipango ya Serikali.

Amewataka viongozi hao wasisubiri Rais aseme Mkuu wa Mkoa fanya hili huko kwani hiyo ilikuwa dhana iliyojengeka zamani.

“Enzi za Mwanri (Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Tabora) mimi napenda kuona mtu anajituma, anajielewa anajua nini anafanya,” amesema na kuongeza;

“Kwenye ndoto zako hizo usiyumbishwe  unatakiwa kuwa na hoja za kujitetea iwapo unachokifanya kitahojiwa,” amesema.

Aidha, amewataka viongozi hao kusimamia maamuzi yao, huku akionya hilo lisiwafanye kutokubali ushauri wa wengine.

“Naposema kusimama kwenye maamuzi yako sio muende huko kichwa ngumu mnachotaka ndo hicho hicho, hapana, unaangalia mazingira yaliyopo na unafanya kulingana na miongozo ya kisheria,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

error: Content is protected !!