Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia amliza mjane wa Magufuli
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia amliza mjane wa Magufuli

Spread the love

MANENO ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, juu ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dk. John Magufuli imemliza  mjane wake, Janeth Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Tukio hilo limetokea jana tarehe 5 Novemba 2023, wakati Rais Samia akizindua nyumba mpya ya Hayati Magufuli ambaye alikuwa mtangulizi wake, iliyojengwa na Serikali, jijini Dar es Salaam.

Mama Janeth alijikuta anaatokwa machozi wakati alipomkumbatia Rais Samia, pia baadhi ya wanafamilia yake walijikuta wakilia wakati kiongozi huyo anatoa hotuba yake.

Wakati akitoa hotuba yake, Rais Samia alimuomba Mama Janeth akubali kupokea nyumba hiyo kwa niaba ya Hayati Magufuli, ambaye amemtaja kama mlezi na kaka yake.

“Ndugu yangu Janeth, nikiwa na mchanganyiko wa hisia naomba leo (jana) uridhie kupokea nyumba hii kwa niaba ya mpendwa wetu, kaka yangu, boss wangu na mlezi wangu, Hayati Magufuli,” alisema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia aliagiza wake wa viongozi ambao wametangulia mbele ya haki, watunzwe kwa kuwa walilitumikia taifa wakati wenza wao wako madarakani.

“Hawa watu ni haki yao watunzwe, walilitumikia taifa wakati waume zao wako kazini na wenyewe walitumikia taifa. Waume wamewaacha ni lazima tuwatunze,” alisema Rais Samia.

Kwa upande wake Mama Janeth, alimshukuru Rais Samia akisema “mheshimiwa Rais tendo ulilofanya litabaki kuwa lililotukuka na alama isiyofutika kioyoni mwetu ukizingatia kuwa nyumba hii itakuwa ndiyo makazi ya kudumu ya familia. Nakushukuru sana mama ubarikiwe.”

“Kitendo hiki ulichotutendea katika familia ya Hayati Magufuli ni dhahiri kwamba umeniachia deni, nikiwa kama mama wa familia hii zawadi pekee ninayoweza kukuahidi ni kukuombea mema daima kwa mola wetu ili Mungu aendelee kukupigania na kukubariki na kukujalia maisha mema na kazi unayofanya,” alisema Mama Janeth

Hayati Magufuli alifariki dunia akiwa madarakani kwa ugonjwa wa umeme, tarehe 17 Machi 2021 na mwili wake ulizikwa kijijini kwao Chato mkoani Geita. Wakati anafariki, Rais Samia alikuwa makamu wake wa Rais.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!