Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia ajitosa sakata la Mbowe ‘mahakama itaamua’
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ajitosa sakata la Mbowe ‘mahakama itaamua’

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewaomba Watanzania na ulimwengu kwa ujumla, kusubiri maamuzi ya mahakama dhidi ya mashtaka yanayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Chadema, Freeman Mbowe. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu, tarehe 9 Agosti 2021 katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) yaliyofanyikia Ikulu ya Dar es Salaam.

Mbowe na wenzake watatu, wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kupanga njama za kufanya ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Rais Samia amesema mahakama hiyo ndiyo itakayothibitisha kama Mbowe ana hatia au hana hatia.

“Kwa sababu jambo liko mahakamani, sina uhuru wa kulizungumzia kwa sana, nadhani tuiachie mahakama ionyeshe ulimwengu hizo shutuma walizomshutumu ni za kweli, au si za kweli. Mahakama itaamua,” amesema Rais Samia

Alipoulizwa kama Mbowe ameshtakiwa kwa makosa hayo kwa sababu za kisiasa, Rais Samia amejibu “mimi sidhani kama yamechochewa kisiasa, kwa sababu  ninavyojua Mbowe alifunguliwa kesi Septemba 2020,  yeye pamoja na wengine na kama ulivyosema mashtaka ya ugaidi na kuhujumu uchumi.”

“Nadhani wengine kesi zao zimesikilizwa,  wengine wamepewa hukumu zao wanatumikia. Yeye upelelezi ulikuwa haujaisha, uchunguzi ulikuwa unaendelea. Kwa hiyo amekwenda tumeingia kwenye uchaguzi,” amesema Amri Jeshi hiyo mkuu.

Freeman Mbowe na wenzake wakiwa mahakamani Kisutu

“Amemaliza uchaguzi,  nadhani sasa Polisi wamekamilisha uchunguzi wao,  wamemhitaji waendele na kazi yao,” amesema Rais Samia.

Kiongozi huyo wa Tanzania, amesema kilichomchelewesha Mbowe kutounganishwa na wenzake katika kesi hiyo ni mwanaasiasa huyo kuwa nje ya nchi.

“Kama utakumbuka Mbowe kipindi kirefu hakuwepo nchini, alikuwepo Nairobi. Kwa nini kakimbia sijui, lakini alivyoingia tu nchini kaitisha maandamano ya madai ya katiba,  nadhani ni mahesabu amejua kwamba ana kesi ya aina hiyo na hii vurugu akikamatwa aseme kwa sababu ya katiba,” amesema Rais Samia.

Mbowe alikamatwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai 2021, alijiandaa kushiriki kongamano la katiba mpya, lililoandaliwa na Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha).

Baada ya kukamatwa Mwanza, Mbowe aliletwa jijini Dar es Salaam, ambapo alipandishwa kizimbani tarehe 26 Julai mwaka huu, na kuunganishwa katika keai ya uhujumu uchumi inayowakabili wengine watatu, ambao walikuwa walinzi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!