May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mnata, Shikalo watemwa Yanga, Haucho atambulishwa

Spread the love

 

MABINGWA wa kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam, imeendelea kujiimalisha kwa msimu wa 2021/22 kwa kumsajili kiungo mkabaji, Kharid Haucho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Haucho, raia wa Uganda ametambulishwa leo Jumatatu, tarehe 9 Agosti 2021 akitokea Misri Lel Makkasa kama mchezaji huru. Amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili.

Huu ni usajili wa tano wa Yanga tangu ilipoanza kusajili. Kati yao wanne ni wa kimataifa akiwemo golipika kutoka nchini Mali, Djigui Diarra.

Wengine; ni mshambuliaji wao wa zamani, Haritier Makambo akitokea Horoya ya Guinea; Fiston Mayele akitokea AS Vital wote raia wa Congo pamoja na mshambuliaji Yusuph Athuman ambaye ni Mtanzania akitokea Biashara United.

Farouk Shikalo, aliyekuwa mlinda mlango wa Yanga

Yanga ambayo imekosa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa msimu wa nne mfululizo, ambapo imeshuhudia watani zao Simba ikilingakua ikiwemo mara mbili la ubingwa wa FA ikiwemo la msimu huu wa kuwafunga wao wenyewe, wamedhamilia kuchukua mataji hayo msimu ujao.

Haucho ametambulishwa leo Jumatatu, tarehe 9 Agosti 2021 na Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa akisema, wanaendelea kufanyia ripoti ya kocha wao ya kusajili wachezaji wenye viwango.

Akizungumza katika utambulisho huo, Haucho amesema, alikuwa na ofa za timu nyingi zikiwemo Simba na Azam “lakini mazungumo yangu na Yanga, yalikuwa kama ya kifamilia, ndiyo nimeamua kujiunga na Yanga.”

Metacha Mnata, aliyekuwa kipa wa Yanga

Wakati huohuo, Katibu mkuu huyo wa Yanga, Mfikirwa amesema, leo alikuwa na mazungumzo na makipa wao, Farouk Shikalo raia wa Kenya na Metacha Mnata ambaye ni Mtanzania ambao ambao wamehitmisha safari yao ya kuitumikia.

“Unajua unaposajili, wengine wanaondoka na makipa wetu Shikalo na Metacha nimekutana nao ili kuwafahamisha ili wajue nini kinaendelea. Tunawashukuru Shikalo na Metacha, tumekaa nao kwa miaka miwili na tumefanya nao vizuri, kama wanavyosema unapokuwa na mwanzo, hukosi kuwa na mwisho. Ni wakati mgumu kidogo na tumemalizana nao,” amesema Mfikirwa

error: Content is protected !!