May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia agonga siku 100 Ikulu

Samia Suluhu Hassan, akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Spread the love

 

LEO Jumapili, tarehe 27 Machi 2021, Samia Suluhu Hassan, ametimiza siku 100 tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Aliapishwa tarehe 19 Machi 2021, Ikulu ya Dar es Salaam na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.

Ni baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, kilichotokea saa 12 jioni ya tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Mwili wa Hayati Magufuli, ulizikwa nyumbani kwao, Chato mkoani Geita.

Hayati John Magufuli

Samia, aliyekuwa makamu wa Rais, aliapishwa kuwa Rais kwa mujibu wa Katiba kisha yeye mwenyewe akamteua Dk. Philip Mpango, aliyekuwa waziri wa fedha na mipango kuwa makamu wa Rais.

Kesho Jumatatu, katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere, Dar es Salaam atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu siku 100 akiwa madarakani.

error: Content is protected !!