Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vyama vya siasa Tanzania vyamsubiri Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Vyama vya siasa Tanzania vyamsubiri Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

VIONGOZI wa vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania, wamemkumbusha Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan, atekeleze ahadi yake ya kuonana nao, ili kuzungumza mustakabali wa hali ya kisiasa nchini humo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa na viongozi hao hivi karibuni, wakizungumza na MwanaHALISI Online, kuhusu siku 100 za Rais Samia tangu alipoingia madarakani, tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Tanzania, tarehe 19 Machi 2021.

Leo Jumapili, tarehe 27 Juni 2021, Rais Samia ametimiza siku 100 tangu aingie Ikulu, kuchukua nafasi ya Dk. John Pombe Magufuli, ambaye alifariki dunia 17 Machi 2021, Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.

Mara baada ya kuingia madarakani, Rais Samia, alitoa ahadi ya kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani, tarehe 22 Aprili 2021, akilihutubia Bunge jijini Dodoma, ili kujenga mazingira mazuri ya kukuza demokrasia.

Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhandisi Mohammed Ngulangwa, amemuomba Rais Samia atekeleze ahadi hiyo, ili kufungua milango ya mashauriano na vyama hivyo.

“Tunamuomba afungue milango ya mashauriano na viongozi wa vyama, ili kujadili namna ya kuboresha hali ya kisiasa nchini,” amesema Ngulangwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe, amesema ni vyema Rais Samia akakutana na vyama vya siasa, ili wamalize changamoto zilizopo katika shughuli za kisiasa nchini.

“ Tunamngojea maana ametuahidi atatuona, atazungumza na sisi. Tunaona muda unazidi kuyoyoma tu, kwa hiyo hatujasema tumekata tamaa,” amesema Rungwe na kuongeza:

“Lakini tunaona muda unakwenda na kutuona hajatuona na watu wa vyama vya siasa ndio sisi, basi nafikiri angepanga vizuri akatuona ili haya mambo yaishe.”

Katibu Mkuu wa Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC) Taifa, Doyo Hassan Doyo, amemuomba Rais Samia atekeleze ahadi yake hiyo.

“Atekeleze ahadi ambayo ameitoa ya kukutana na vyama vya siasa kuzungumzia hatma ya demokrasia,” amesema Doyo.

Aidha, Doyo amesema, katika siku 100 za uongozi wa Rais Samia, hali ya vyama vya siasa imeanza kuimarika, kwa kuwa vimeanza kufanya shughuli zake bila vikwazo.

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema (katikati) akiwasili uwanja Ndege JK Nyerere. Kushoto Freeman Mbowe na John Mnyika (kulia).

“Hali ya vyama vya siasa katika siku 100, imeanza kuimarika. Ni nzuri kwa sababu leo tunafanya siasa, mfano chama chetu cha ADC tumefanya ziara katika mikoa sita bila kuzuiwa,” amesema Doyo na kuongeza:

“Na vyama vingine viko mikoani vinafanya siasa, wengine wako Dar es Salaam wanafungua matawi. Utaona namna gani hali ya kisiasa katika siku 100 za Rais Samia imeimarika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!