KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka wabunge wanaotokana na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), kusimamia kwa karibu utolewaji wa fedha za mikopo ya wanawake katika halmashauri zote nchini.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi 26 Juni 2021, wakati akifungua kikao cha kawaida cha Baraza Mkuu la UWT kilichofanyika katika ukumbi wa NEC, makao makuu ya chama hicho.
“Wabunge wa UWT wote, wakae na waandike taarifa kwenye kila maeneo yao wanapotoka au mkoa kuhusu asilimia nne (4%) ya fedha za halmashauri walivyozisimamia na zilivyoleta tija katika eneo hilo kwa wanawake.
“… lakini na namna walivyowasilisha kwenye vikao vyao ngazi ya wilaya na mikoa ili kuleta muunganiko na usimamizi wa karibu wa fedha hizi,” amesema Chongoli.
Aidha, pamoja na mambo mengine, Chongolo amesisitiza viongozi wote wa UWT kuweka mkazo katika kukutana na kufanya vikao kuanzia ngazi za matawi walipo wanachama na wananchi na kwamba, kwenye vikao hivyo ajenda ya kudumu iwe ni fursa za wanawake.
Leave a comment