December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aanika idadi ya majengo, yapo ya shule na afya

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

NCHI ya Tanzania, ina majengo 14,348,372 (milioni 14.3), ambapo Bara kuna majengo 13,907,951 na Zanzibar 440,421. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumatatu, tarehe 31 Oktoba 2022, jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan, akitangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi ya 2022, iliyofanyika Agosti mwaka huu.

Rais Samia amesema, majengo ya kutolea huduma za afya yako 10,067, kati ya hayo 7,889 ni ya zahanati, wakati ya vituo vya afya yakiwa 1,490 huku ya hospitali yakiwa ni 688.

“Upande wa elimu, matokeo yanaonyesha Tanzania ina jumla ya shule 25,626, ambapo shule za msingi ni 19,769 na shule za sekondari ni 5,857. Ndugu wananchi idadi yetu kwa sasa ni kama nilivyotaja,” amesema Rais Samia.

Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi iliyotangazwa na Rais Samia, majengo hayo yanahudumia watu 61,741,120.

error: Content is protected !!