Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT
Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati ya pamoja kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mashamba makubwa ya pamoja katika Program ya Bulding Better Tomorrow (BBT), ili usikwame. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo leo tarehe 20 Machi 2023, akizindua mradi huo awamu ya kwanza, jijini Dodoma.

“Lakini nisisitize kama alivyosema spika, kwamba suala hili la kitaifa na sio suala la wizara ya kilimo peke yake, watu wa maji, umeme, ardhi na mazingira watahusika, sekta mbalimbali zitahusika. Niombe mawaziri wangu kama hamna kamati mkaunde mtakaoshughulikia jambo hili, sitaki kusikia kushindwa lazima tufanikiwe,” amesema Rais Samia.

Amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya kilimo hususan kwa kuendelea kuajiri watalaamu ikiwemo watumishi wa sekta ya umwagiliaji.

“Katika kuimarisha huduma za ugani, tutaendelea kutenga bajeti mahususi kwa ajili ya ajira mpya za watumishi wa sekta ya umwagiliaji maji. Tumeajiri 300 na tutaendelea kukupa wataalamu ili mwende mkafanye kazi huko wanakotakiwa. Tutaendelea kutoa ajira ili vijana waweze kuwa wengi zaidi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema dhamira yake ni kuhakikisha kilimo kinakuwa cha biashara lakini pia mchango wake katika pato la taifa unaongezeka kutoka asilimia 3 iliyokuwa sasa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo 2025.

Aidha, Rais Samia ameagiza vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya utekelezaji wa BBT, vitumike kwa wakulima waliopembezoni mwa mashamba hayo.

Awali, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alisema vijana takribani 800 watanufaika na mradi huo katika awamu ya kwanza.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!