Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani
Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
Spread the love

 

WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari imegawa pikipiki 5,500 kati ya 7000 zilizonunuliwa kwa ajili ya maafisa ugani kusimamia shughuli za kilimo katika kila Kata. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ … (endelea).

Ameyasema hayo leo tarehe 20 Machi 2023 katika uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja ikiwa ni utekelezaji wa programu ya Building Better Tomorrow, iliyofanyika jijini Dodoma mgeni rasmi akiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Pia Bashe amemuonesha Rais mfumo wa teknolojia ya namna ambavyo wanaweza kudhibiti maafisa ugani ambao walipewa vitendea kazi kama pikipiki wasiweze kutoka nje ya maeneo yao ya kazi.

Sambamba na hilo amezungumzia miradi ya mabwawa ya umwagiliaji iliyopo katika maeneo mbalimbali ambayo inaendelea na ujenzi kwa ajili ya kupata maji yatakayotumika katika shughuli za kilimo kwa ajili ya umwagiliaji.

“Lakini pia kuna mradi wa block farming wa Membe ambao shughuli za ujenzi zinaendelea, mradi huu utatugharimu Sh 32 bilioni mpaka utakapokamilika, na una jumla ya hekari 8,000,” amesema Bashe.

Ikiwa ni moja ya shughuli za kilimo, Bashe amemuonesha Rais Samia jinsi shughuli za upuliziaji wa viuatilifu kwa mimea kwa kutumia ndege zisizo na rubani ‘drones’ ambazo zitaweza kurahisisha shughuli za unyunyuziaji wa viuatilifu kwa mimea.

“Kuna maeneo sio rahisi kuzuia vimelea vya magonjwa kwa mimea, kwahiyo tumeanza kutumia drones ambazo zitarahisha shughuli za upuliziaji wa mimea kwa urahisi,” amesema Bashe.

1 Comment

  • CANADA Embassy and TACAIDS Here by requesting Trillion USD 56 to finance spread of diseases like HIV, Gonorea and Hapetititis B

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!