Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mkapa awakutanisha Maalim Seif, JPM
Habari za Siasa

Rais Mkapa awakutanisha Maalim Seif, JPM

Spread the love

RAIS John Magufuli amekutaa uso kwa uso na Maalim Seif Sharif Hamad, kwenye uzinduzi wa kitabu cha Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Maalim Seif, ambaye alikuwa mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amekuwa akikosoa utawala wa Rais Mkapa hususan mwenendo wa demokrasia nchini.

Rais Mkapa anazinduia kitabu chake kiitwacho ‘Maisha Yangu, Kusudio Langu’ leo tarehe 12 Novemba 2019, katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo unafanyika leo ambayo ni siku ya kuzaliwa Rais Mkapa. Alizaliwa mwenzi na tarehe ya leo miaka 81 iliyopita katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.

Rais Mkapa alikuwa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa wa Awamu ya Tatu, kuanzia mwaka 1995 – 2005. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Rais Magufuli.

Kwenye uzinduzi huo, viongozi mbalimbali wamehudhuria wakimwemo marais wastaafu Alhaji Alli Hassan Mwinyi (Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili) na Rais Jakaya Kikwete (Awamu ya Nne).

Wengine waliohudhuria ni Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar, Job Ndugai, Spika wa Bunge; Profesa Ibrahim Juma, Jaji Mkuu wa Tanzania; Jaji Mkuu Mstaafu na Othman Chande.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!