Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli awashukuru wazee wa Nachingwea
Habari za Siasa

Rais Magufuli awashukuru wazee wa Nachingwea

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli amewashukuru wazee wa Nachingwea Mkoa wa Lindi kwa mchango wao wa Sh. 100,000 walioutoa ili umsaidie katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Nachingwea … (endelea).

Julai 13, 2020 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Nachingwea alipokea mchango huo kwa niaba ya Rais Magufuli kutoka kwa wazee hao.

Akitoa salamu hizo kwa niaba ya Rais Magufuli, leo mchana Jumanne tarehe 21 Julai 2020, katika uwanja wa ndege wa Nachingwea mkoani Lindi,  Majaliwa amesema Rais Magufuli amefarijika sana kwa mchango huo.

“Rais amesema, aliniona wakati napokea salamu kutoka kwa wazee hapa uwanja wa ndege Nachingwea, mkanikabidhi mchango kwa ajili yake, anawashukuru sana na salamu zenu amezipokea kwa mikono miwili,” amesema.

Amesema Rais Magufuli anawashukuru kwa kupata wazo hilo na amewataka waendelee na majukumu yao na ameahidi kuzunguka maeneo yote nchini ili kuwapa mrejesho wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020.

Akizungumzia mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM, Majaliwa amewapongeza wana CCM waliojitokeza kwa wingi kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na amewataka  waendelea kuwa wamoja.

“Endeleeni kuwa wamoja hata baada ya mchakato wa kumpata mgombea mmoja wa kupeperusha bendera ya CCM kukamilika na ninawasihi wote muungeni mkono mgombea huyo ili kujenga mshikamano na kukipa chama ushindi,” amesema.

Majaliwa amesema hayo baada ya kubaini miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea kumuaga wakati akitoka Ruangwa kurejea Dodoma ni Wana CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya chama kwa nafasi ya ubunge na ambao wamemaliza mchakato wa awali wa kupigiwa kura.

 Wakati huohuo, Majaliwa amewataka viongozi wa chama na Serikali wahakikishe wanawahamasisha wananchi kufanya kazi za kujiletea maendeleo ikiwemo kujihusisha kwenye kilimo na biashara.

“Ndugu zangu, tuendelee kuhamasisha Watanzania na wana- Nachingwea wafanye kazi kwa bidii, lazima kila kaya ijiridhishe, inakuwa na chakula cha kutosha lakini pia ilime mazao ya kibiashara kama korosho, ufuta, alizeti na mazao mengine, kila mmoja awe na akiba ya kutosha ya mazao ya chakula na biashara.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!