Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli apingwa mahakamani
Habari za Siasa

Magufuli apingwa mahakamani

Spread the love

FATMA Karume, Wakili na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) anaongoza mawakili wenzake upande wa mashtaka kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu Serikali (AG), Dk. Adelardus Kilangi uliofanywa na Rais John Magufuli. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT -Wazalendo ndiye aliyefungua madai hayo ambayo yameanza kusikilizwa leo tarehe 7 Februari mwaka 2019.

Madai hayo yamefunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo Ado anapinga utaratibu uliotumika kuteuliwa Dk. Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jopo la Majaji wanaosikiliza kesi hiyo ni pamoja na Jaji Kiongozi Dk.  Dk Eliezer Felishi, Dk Benhajj Masoud na Jaji Luvada.

Kwenye kesi hiyo namba 29 ya mwaka 2019 Ado ameiomba mahakama mambo matatu ;- Mahakama itamke kuwa Rais Magufuli amevunja Katiba kwa kumteua Dk Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu, mahakama itamke kuwa Dk. Kilangi amevunja Katiba kwa kukubali kuteuliwa na Rais Magufuli kinyume na Katiba na pia mahakama itamke kuwa uteuzi huo sio halili na ni uvunjifu wa Katiba ya Nchi.

Mahakama imeipa serikali siku 14 kujibu mashtaka ya Ado. Shauri hilo limeahirishwa mpaka tarehe 22 Februari mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza majibu ya serikali juu ya mashaka hayo.

Rais Magufuli alimteua Dk. Kilangi kushika wadhifa huo tarehe Mosi Februari 2018. Kabla ya kuteuliwa kwake, alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu cha Arusha pia alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!