Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Mahakama yamkubalia Mdee shingo upande
Habari Mchanganyiko

Mahakama yamkubalia Mdee shingo upande

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imekubali shingo upande sababu za Halima Mdee, Mbunge wa Kawe kushindwa kuhudhuria kesi yake leo 7 Februari 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Mdee alitakiwa kuhudhuria kesi yake ya kutoa lugha chafu kwa Rais John Magufuli kwa madai ya kumuuguza mbunge mwenzake Ester Bulaya (Bunda Mjini) mkoani Dodoma. 

Kutoka na taarifa hiyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Mdhamini wa Mdee, Faris Lupomo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba alitaja sababu hiyo wakati kesi hiyo ilipoletwa kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Simba amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini huyo kuhusu kushindwa kufika mahakamani kwa mshtakiwa zinaleta ukakasi na kubainisha kuwa, zina lengo la kuifanya kesi hiyo isimalizike kwa wakati.

Hakimu huyo amesema, madaktari na wabunge wengine wanawake ambao wanaweza kumuuguza Bulaya wapo na kwamba, mahakama ikiruhusu hayo yaendelee kesi itashindwa kumalizwa.

“Kiukweli jambo hili linakwaza na linatia wasiwasi kama hii kesi tutaweza kumaliza kwa mwendo huu, tunakubali sababu hiyo ya kuuguza lakini kwa shingo upande.

Hata hivyo Lupomo amedai, aliwasiliana na mbunge huyo na kumueleza kuwa atashindwa kufika mahakamani kwa kuwa, anamuuguza Bulaya katika Hospitali ya Bunge mkoani Dodoma.

Wakili wa Utetezi Hekima Mwasipu naye alikiri mahakamani hapo kwa mshtakiwa huyo hayupo na amepewa taarifa na mdhamini huyo kuwa, anamuuguza Bulaya mjini Dodoma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi 28 Februari mwaka huu. Mpaka sasa mashahidi watatu wameishatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu wa Polisi Batseba Kasanga.

Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo tarehe 3 Julai 2017 akiwa katika ofisi za Chadema zilizopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Anadaiwa kutamka “anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge breki” na kudaiwa kitendo hicho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!