April 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli ‘aisuka’ NEC

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli, amemteua Wilson Charles kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Charles amechukua nachukua nafasi ya Athuman Kihamia, aliyekuwa mkurugezi wa tume hiyo na kwamba atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa ya Kihamia kung’olewa NEC, imetolewa leo tareje 1 Oktoba 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa.

Kwenye taarifa hiyo, Rais Magufuli amemteua Kanali Wilbert Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Charangwa Selemani ameteuliwa kuwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala huku Thomas Salala akiwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara.

Pia taarifa hiyo imebeba uteuzi wa wakurugenzi 10 ambapo Rehema Bwasi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, awali alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Korogwe, Tanga.

Ezekiel Magehema ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela. Kabla ya uteulizi huo alikuwa Ofisa Tarafa wa Malangali, Iringa.

Ndaki Muhuli ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Walaya ya Siha mkoani Kilimanjaro. Awali alikuwa Katibu Tawala Wilaya ya Kitero, Manyara.

Sheillah Lukuba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Awali alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Said Magaro ameTEULIWA kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Tabora. Awali alikuwa Ofisa Tarafa wa Msota, Pwani.

Mohamed Mavura ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Pwani. Awali alikuwa ofisa katika Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Diana Zacharia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Mara. awali alikuwa ofisa tarafa Ukerewe, Mwanza.

Hanji Godigodi amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Songwe. Awali alikuwa Ofisa Elimu Taaluma, Dar es Salaam.

Godwin Chacha ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Kilimanjaro. Awali alikuwa Ofisa Tarafa wa Maswa, Simiyu.

Hawa Mposi amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Morogoro. Awali alikuwa Ofisa Tarafa wa Ifakara, Morogoro.

error: Content is protected !!