April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM asaini sheria nne mpya

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli amesaini sheria nne zilizopitishwa katika mkutano wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 1 Oktoba 2019 na Ofisi ya Bunge kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Taarifa hiyo ya Bunge inaeleza kuwa, sheria hizo zimetangazwa katika Gazeti la Serikali, na zinapatikana katika tovuti rasmi ya mhimili huo.

Sheria zilizosainiwa ni, Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 4) Sheria Namba 11 ya mwaka 2019.

Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mablimbali (Na. 5) Sheria Na. 12 ya mwaka 2019 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) Sheria Na. 13 ya mwaka 2019.

error: Content is protected !!