Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Dk. Mwinyi kumwaga bilioni 460 mtaani, awapiga dongo wanaomkejeli uchumi wa bluu
Habari za SiasaTangulizi

Rais Dk. Mwinyi kumwaga bilioni 460 mtaani, awapiga dongo wanaomkejeli uchumi wa bluu

Spread the love

 

RAIS wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema katika mwaka wa pili wa uongozi wake ataingiza Sh bilioni 460 katika mzunguko wa kiuchumi ili kila mtu anufaike. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Pia amesema watu wanaomkejeli kuhusu kuujenga uchumi wa blue, katu hatovunjika moyo wala kukata tamaa kwani nia njema huonekana asubuhi.

Rais Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Novemba, 2021 katika kilele cha Sherehe za Mwaka mmoja tangu alipoingia madarakani.

Akizungumza katika sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Abed Karume Visiwani Zanzibar, Dk. Mwinyi amesema mwaka wa kwanza ulikuwa mgumu kutokana na mdororo wa kiuchumi.

Amesema fedha hizo ni nyingi na zitagusa sekta zote kuanzia kwenye sekta ya ujenzi na kunufaisha watu wengi.

“Ni mategemeo yangu kuwa mwaka wa pili wa serikali awamu ya nane utakuwa na mafanikio zaidi,” amesema.

Amesema Sh bilioni 230 za mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha Duniani (IFM) zinazolenga kukabiliana na athari za ugonjwa wa Covid- 19, zitaelekezwa kwenye maeneo maalumu matano.

“Kwa sababu fedha za IMF bilioni 230 zina masharti, tutaziingiza kwenye sekta tano za afya, elimu, maji, umeme na kuwawezesha wajasiriamali,” amesema.

Aidha, amesema Serikali itakopa fedha kama hizo Sh bilioni 230 kuimairisha sekta na maeneo mengine ambayo hayapo kwenye mpango wa fedha za IMF.

“Kuendelea kufufuka kwa uchumi wa dunia na uchumi wetu hasa sekta ya utaliii kunanipa imani kubwa kwamba tuna uwezo wa kuhimili mkopo huu ili tuweze kufanya mambo mengine makubwa kwa wananchi wetu.

“Tutazitumia kuongeza mzunguko wa fedha kwa wafanyabiashara na wananchi, katika mwaka wa pili wa uongozi wangu nataka kuhakikisha tunalipa madeni makubwa ambayo serikali inadaiwa na wazabuni, malipo ya fidia za mali za wananchi, wastaafu na wafanyakazi wa serikali,” amesema

Amesema madeni ya malipo ya ndani sasa yamefikia Sh bilioni 68.2.

“Nimeamua kufanya hivyo, nikiamini kwamba Serikali inapochelewesha madeni ya wazabuni na wafanyabiashara, inaathiri ukuaji wa biashara na mzunguko wa fedha. Tukiwa na mipango imara ya kulipa madeni haya shughli nyingi za kijamii zitaimarika,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

ACT-Wazalendo yasusia uchaguzi wa ubunge Zanzibar

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo, kimegoma kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo...

error: Content is protected !!