May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vidonge vinavyoweza kutibu Corona vyagundulika

Spread the love

 

WAKATI nchi mbalimbali duniani zikiendelea kuagiza mamilioni ya chanjo dhidi ya Virusi vya Corona, sasa vimepatikana vidonge vyenye uwezo wa kutibu ugonjwa wa Covid kwa zaidi ya asilimia 89. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kidonge cha majaribio cha kutibu Covid kilichotengenezwa na kampuni ya Pfizer ya nchini Marekani kinapunguza hatari ya kulazwa au kifo kwa asilimia 89 kwa watu wazima walio hatarini.

Dawa hizo zilizopewa jina la Paxlovid – inakusudiwa kutumika mara tu mtu anapopata dalili kwa wale ambao wako hatari kubwa ya ugonjwa huu.

Hatua hiyo imekuja ikiwa imepita siku moja baada ya mamlaka ya dawa nchini Uingereza kuthibitisha tiba inayofanana na hiyo kutoka Merck Sharp na Dohme (MSD).

Pfizer inasema imeacha kufanya majaribio mara tu walipopata matokeo chanya ya dawa hiyo.

Uingereza imeagiza dozi 250,000 za dawa za Pfizer na dawa 480,000 za vidonge vya MSD molnupiravir.

Dawa hizi mgonjwa anakunywa vidonge vitatu kwa siku kwa kipindi cha siku tano.

error: Content is protected !!