Friday , 17 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Mwinyi aeleza hali ya uchumi wa Zanzibar
Habari za Siasa

Rais Mwinyi aeleza hali ya uchumi wa Zanzibar

Spread the love

 

KASI ya ukuaji uchumi wa Zanzibar, imeshuka kutoka asilimia 7.7 iliyokuwa 2019, hadi kufikia asilimia 1.3 mwaka jana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 6 Novemba 2021, visiwani Zanzibar na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwingi, akihutubia katika sherehe za kuazimisha mwaka mmoja tangu alipingia madarakani tarehe 2 Novemba 2020.

“Mwaka 2020 kasi ya ukuaji uchumi Zanzibar, ilishuka hadi asilimia 1.3, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.7, ya mwaka 2019,” amesema Rais Mwinyi.

Rais huyo wa Zanzibar, amesema changamoto hiyo imesababishwa na mlipuko wa janga la Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19), uliotokea mwishoni mwa 2019.

Amesema, baada ya UVIKO-19 kuingia, sekta ya utalii ambayo ni kitovu cha uchumi wa visiwa hivyo, iliporomoka, idadi ya watalii walioingia Zanzibar ilipungua kwa asilimia 51.6, kutoka 538,000 mwaka 2019, hadi kufikia 260,000 (2020).

“Takwimu zinaonesha asilimia 95 ya hoteli ziliopo Zanzibar, zenye nyota kuanzia moja hadi tano, zilifungwa au kupunguza shughuli za uzalishaji kuanzia 2020 na kupelekea kupungua wafanyakazi kwa asilimia 90,” amesema Rais Mwinyi.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, amesema kuporomoka kwa sekta ya utalii kumeathiri maendeleo ya ukuaji wa sekta nyingine.

Rais huyo wa awamu ya nane Zanzibar, ametaja sekta zilizoathirika na ugonjwa huo, ikiwemo viwanda ambayo mauzo ya bidhaa laini kama maji na soda, yalishuka kwa zaidi ya asilimia 90, kutokana na kupungua kwa mahitaji sokoni kulikosababishwa na kufungiwa kwa hoteli.

“Takwimu zinaonesha uingizwaji bidhaa kutoka nje ya nchi, ulipungua kwa asilimia 44.2, kwa upande wa usafiri wa anga idadi ya ndege za kimataifa 2020, ilishuka hadi kufikia 605 kutoka 1,834 (2019),” amesema Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi amesema “wakati idadi ya ndege za ndani 2020 ilishuka kufikia 2,563, kutoka 4632 (2019), hivyo makusanyo ya mapato katika uwanja wa ndege yakapungua kwa zaidi ya asilimia 80 na kupelekea mamlaka ya viwanja vya ndege Zanzibar, kushindwa kumudu huduma zao za msingi.”

Rais Mwinyi amesema, changamoto za UVIKO-19 katika uchumi wa Zanzibar, zimesababisha kupanda kwa gharama za bidhaa, kupungua kwa mzunguko wa fedha katika uchumi.

Na kuongezeka kwa mfumuko wa bei, vitendo vilivyopelekea ugumu wa maisha kwa wananchi.

“Kutokana na athari hizo za kiuchumi, maisha na kipato cha wananchi kiliathirika hususan na ongezeko la bei ya bidhaa tunazoziagiza kutoka nje ya nchi, hasa za vyakula na nishati za mafuta,” amesema Rais Mwinyi.

Kufuatia changamoto hizo, Rais Mwinyi amesema Serikali yake inaendelea kuchukua jitihada za kuimarisha uchumi wa Zanzibar, ikiwemo kuongeza mzunguko wa fedha kwa kutumia mikopo yenye masharti nafuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yatoa kauli wanaolala nje Hospitali ya Muhimbili

Spread the loveSERIKALI imesema inajipanga kushirikiana na sekta binafsi kujenga majengo yatakayosaidia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!