Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Profesa Mkenda kuwatumia wastaafu kuboresha elimu Tanzania
HabariHabari za Siasa

Profesa Mkenda kuwatumia wastaafu kuboresha elimu Tanzania

Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu
Spread the love

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ProfesaAdolf Mkenda amesema atatenga muda wa wiki tatu kuzungumza na watumishi wa wizara hiyo na kupitia nyaraka muhimu za wizara lengo likiwa ni kufanya uchambuzi wa kuboresha elimu ili iwe yenye tija. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Amesema, hataona shida kuwatafuta wataalamu wabobezi wa elimu wakiwemo wastaafu ili kuweza kupata mchango wao wa kuboresha elimu ya Watanzania kwa manufaa ya Taifa.

Profesa Mkenda amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 13 Januari 2022, jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya ofisi kutoka kwa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Profesa Joyce Ndalichako.

Ni baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Profesa Mkenda amehamishiwa wizara hiyo kutoka wizara ya kilimo na Profesa Ndalichako aliyeongoza wizara ya elimu toka Desemba 2015, akihamishiwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu.

Profesa Mkenda amesema, wizara hiyo ni wizara nyeti hivyo inatakiwa kuitendea haki kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watumishi.

“Wizara hii siyo ya kuchezea ni wizara nyeti sana na ukiichezea inahitaji siyo kubadilisha badilisha mambo kwa kubadilisha mambo tutalichanganya taifa,” amesema Profesa Mkenda ambaye ni Mbunge wa Rombo, Kilimanjaro

“Pia ili kuweza kufanya kazi vizuri, naomba ushirikiano na msiwe na nidhamu ya uwoga pale mnapoona kuwa siyo msisite kuniambia ukweli kwani nyie ni wazoefu wa wizara hii muhimu,” amesema

Profesa Mkenda amesema, “tunatakiwa kufanya kazi kama timu, mimi ni waziri lakini hata pale ambapo naona kuwa kutakuwa na tatizo au nikaonekana kukomaa naomba nifuate niambie hapa panahitajika kufanyika jambo fulani.”

Sambamba na hilo, waziri huyo amesema katika kuiboresha elimu ya Kitanzania haoni shida kuwatafuta wataalamu wa elimu kukaa nao kwa nia ya kutoa mchango wao wa kuboresha elimu.

Kwa upande wake, Profesa Ndalichako amesema wizara hiyo ni muhimu hivyo watumishi wanawajibu mkubwa wa kushirikiana zaidi na waziri.

Amesema anakabidhi wizara hiyo kwa waziri mgeni ambaye hana shaka naye katika utendaji huku kukiwa na mipango mbalimbali ambayo anauhakika ataiendeleza.

“Kwanza kabisa naomba kuwashukuru watumishi wenzangu kwa ushirikiano wenu mlionipa na ninaomba mmpe hata waziri wenu Profesa Mkenda,” amesema na kuongeza:

“Ninaondoka huku tukiwa na mipango mbalimbali ya kuifanikisha elimu ya misingi, shule shikizi, sekondari, elimu ya juu na vyuo vya ufundi na amini kabisa mtaendelea na mipango hiyo pamoja na mingine kwa ajili ya kuboresha elimu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariHabari Mchanganyiko

CRB yashtukia makandarasi wanaofanya ubia wa ujanja ujanja, yasema watakaobainika kuchukuliwa hatua kali

Spread the love  BODI ya Usajili wa Makandarasi (CRB), imeonya makandarasi wanaofanya...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Habari

Mnyika aacha ujumbe msibani kwa kada wa Chadema aliyefia vitani Ukraine

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Taifa, John...

error: Content is protected !!