Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Biashara NBC yahitimisha kampeni ya ‘Vuna Zaidi Na NBC Shambani’ kwa mafanikio
Biashara

NBC yahitimisha kampeni ya ‘Vuna Zaidi Na NBC Shambani’ kwa mafanikio

Meneja Masoko wa Benki ya NBC, BAlina Kimaryo (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ iliyokuwa ikiendeshwa na benki benki hiyo kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa uendeshaji wa droo ya mwisho ya kampeni hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Meneja Mahusiano wa Huduma hiyo kutoka benki ya NBC, Ally Abdul (Kulia) na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Neema Tatock.
Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendesha droo yake ya mwisho ya kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ huku ikijivunia kuhitimisha kampeni hiyo kwa mafanikio makubwa ikiwemo kuongeza asilimia 40 ya wateja wa akaunti hiyo ambao ni wakulima wa zao la korosho kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara. Anaripoti mwandishi Wetu … (endelea).

Ikiwa imedumu kwa kipindi cha miezi mitatu kampeni hiyo ilikuwa ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo wa kujidhatiti kwenye kuinua kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la Korosho kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara sambamba na kuongeza wigo wa wateja wake hususani wakulima.

Akizungumza wakati wa uendeshaji wa droo hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Kimaryo alisema benki hiyo imeridhishwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wakulima wa korosho katika mikoa hiyo wakati wote wa kampeni hiyo ambayo pia ililenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa wakulima hao.

Meneja Mahusiano wa Huduma ya NBC Shambani kutoka benki ya NBC, Peter Mbezi (Kulia) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo kwa wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa uendeshaji wa droo ya mwisho ya kampeni hiyo iliyofanyika mwanzoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Kimaryo (Kushoto) na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Neema Tatock (katikati)

“Kampeni hii imekuwa ni yenye mafanikio kwa kuwa imepokewa kwa mwamko mkubwa na walengwa wetu na hivyo kutupa ongezeko la asilimia 40 ya wateja wapya wa akaunti yetu ya NBC Shambani ambao ni wakulima wa korosho katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Hatua hii tumeitafsiri kuwa ni mafanikio makubwa kwa kuwa si tu kwamba imetuwezesha kuongeza wateja bali pia tumefanikiwa kwa vitendo kuunga kwa adhma ya serikali ya kuzalisha tani 700,000 za zao hilo kwa mwaka ifikapo mwaka 2025,’’ alisema

Kwa mujibu wa Alina kupitia kampeni hiyo, benki hiyo imefanikiwa kuongeza elimu ya nidhamu ya fedha miongoni mwa vyama vya ushirika na wakulima kwa ujumla kupitia mafunzo yaliyotolewa na benki hiyo kuhusu umuhimu wa kujiwekea akiba, matumizi ya bima mbalimbali ikiwemo bima ya afya pamoja na kuwekeza kwenye zana za kisasa za kilimo.

Aidha akitangaza washindi kwenye droo hiyo ya mwisho Bi Alina alisema jumla ya washindi 15 walipatikana kupitia droo hiyo wakijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa mikorosho, guta (Toyo) pamoja na zawadi za nyingine ikiwemo kanga, mabegi ya shule na madaftari na hivyo kufanya jumla kuu ya washindi wa kampeni hiyo kuwa ni106 ambao waliweza kupata zawadi hizo zenye thamani ya zaidi ya sh mil 300.

“Kampeni hii itaitimishwa rasmi kwa kuwakabidhi washindi wetu hawa zawadi zao huko huko walipo mwishoni mwa wiki hii. Hatujaishia tu kwenye kutoa zawadi hizi kwenye kampeni hii bali pia kupitia akaunti ya NBC Shambani wateja wetu wataendelea kufurahia faida nyingine nyingi ikiwemo kuweka fedha zao bila makato yoyote zaidi wataendelea kupata kupitia akiba hizo,’’ alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

Biashara

Mchezo mpya mjini Super Heli Kasino, ushindi, zawadi ndiyo sehemu yake

Spread the love  KUNA watu wanakwambia hakuna njia rahisi ya mafanikio kwenye...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yafuturisha Unguja, Pemba, SMZ yaahidi ushirikiano

Spread the loveBENKI ya NMB imeendeleza utamaduni wa kufuturisha wateja wake walioko...

error: Content is protected !!