Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba: CCM bila dola haipo
Habari za Siasa

Prof. Lipumba: CCM bila dola haipo

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) amesema, Watanzania wamechoshwa na maisha ya umasikini, na sasa uhai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kubaki madarakani unategemea hisani ya dola. Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020, wakati wa kufungua Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho wa kuchagua wanachama watakaogombea urais Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar kupitia chama hicho, katika Ukumbi wa Golden Memory Sinza (Mori), jijini Dar es Salaam.

“Ufisadi na rushwa vimeendelea kuimarika nchini na CCM imegawika mapande mapande. CCM sio chama cha siasa bali ni chama dola, bila dola CCM itasambaratika,” Prof. Lipumba amewaambia wajumbe wa mkutano huo akisistiza imebaki kazi ndogo kuiondoa madarakani.

Amesema, Watanzania hawapaswi kutoa fursa kwa CCM kutawala na kuwa, watajuta iwapo wataruhusu chama hicho kuendelea kushika dola.

“Watanzania tutajuta ikiwa tutaruhusu ufisadi mkubwa na wizi wa kura kuipa fursa CCM kuendelea kutawala. CCM haina lengo la kujenga demokrasia ya wananchi.

“Uongozi wa awamu ya tano umeshindwa kuwashirikisha wengine katika uchambuzi wa sera, kubaini matatizo na upimaji utekelezaji, inafanya maamuzi kwa kukurupuka,” amesema Prof. Lipumba.

Kwenye hotuba yake ya ufunguzi, mwanasiasa huyo mtaalamu wa uchumi amesema, Tanzania umasikini umeongezeka, ajira zimetoweka na mafisadi waliostahili kufikishwa katika Mahakama ya Ufisadi, wanajisafisha kwa kubadili vyama.

Amesema, tangu kupatikana Uhuru, sera za chama tawala zimeshindwa kuiondoa Tanzania kwenye lindi la umasikini licha ya kuwa na rasilimali za kutosha.

Pia, amelaumu tabia ya Serikali ya Awamu ya Tano kushindwa kufuata utaratibu wa matumizi na bajeti ya serikali, na kwamba miradi mingine imekuwa ikianzishwa katikati ya mwaka wa fedhe bila kupata idhini ya Bunge hivyo kwenda nje ya mstari wa utawala bora.

“Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa haifuati sheria na taratibu. Utekelezaji wa mambo makubwa unaanza kutekelezwa bila fedha za utekelezaji kuidhinishwa na Bunge. Ndani ya serikali hata Baraza la Mawaziri hakuna mijadala iliyo huru na wazi, uwoga wa wakati wowote unaweza kutumbuliwa umetawala,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!