May 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Lipumba asimulia mwaka 1995 alivyoitwa Profesa uchwara

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF)

Spread the love

MWAKA 1995, niliitwa Profesa uchwara, zile sera za Chama cha Wananchi (CUF), sasa wanazitekeleza lakini wanashindwa kutekelza kwa ufasaha wake kwa kuwa sio zao. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 na Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF Taifa mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa kuchagua mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na visiwani Zanzibar kwenye uchaguzi mkuu Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

“Kwenye sera zetu mwaka 1995, sisi tulisema elimu itakuwa bure na mambo mengine. Haya tumezungumza tangu mwaka huo, niliitwa Profesa uchwara, leo zile sera tulizokuwa tunapigia debe zimechukuliwa moja baada ya nyingine, kwa kuwa sio sera zao wamekuwa wakishindwa kuzitekeleza, tunahitaji kuingia kwenye serikali ili tuzitekeleze,” amesema.

Amesema, sera za elimu bure, afya na mambo mengine muhimu kwa Watanzania, yaliandaliwa mkakati mzuri na chama hicho na kwamba, wale waliokuwa wanabeza ndio hao hao wameingia kutekeleza kwa kiwango hafifu.

Prof. Lipumba amesema, Watanzania kwa sasa hawana furaha, wamepoteza matumaini kutokana na matatizo yao kutotatuliwa na sasa chama hicho ndio kinaweza kurejesha furaha hiyo.

“Tangu mwaka 2012, taarifa ya furaha Duniani ya World Hapinnes Report inaonesha, Tanzania ni ya 148 kati ya nchi 153 kwa kuwa na furaha duniani. Watanzania hatuna furaha kwa sababu ya hali ngumu ya maisha, huduma mbovu za afya, mazingira ya kutoaminiana, uvunjifu wa haki za binadamu, ukosefu wa uhuru na utawala bora,” amesema.

Amesema, Tanzania imerejesha mfumo wa vyama vingi tangu uchaguzi mkuu wa kwanza mwaka 1995 lakini CCM imeendelea kutawala huku wananchi wakiendelea kuteseka kutokana na matatizo yao kuendele kuongezeka.

“Hali hii imewafanya wananchi wengi hasa vijana na wanawake kuwa katika shauku kubwa ya kuoina utawala wan chi yetu unabadilishwa kwa amani,” amesema.

error: Content is protected !!