November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Lipumba amng’oa kigogo CUF

Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera wa chama hicho, Habibu Mnyaa, huku sababu ikitajwa kuwa ni masuala ya uwajibikaji na nidhamu ndani ya chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa ya utenguzi huo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 24 Novemba 2022 na Prof. Lipumba.

Taarifa ya Prof. Lipumba imesema, uteuzi wa kujaza nafasi hiyo utafanyika hivi karibuni.

“Tarehe 28 Aprili 2019 nilimteua Mohamed Habibu Mnyaa, kuwa Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera na alithibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa. Kwa kuzingatia uwajibikaji na nidhamu ndani ya Chama,” imesema taarifa ya Prof. Lipumba na kuongeza:

“Leo tarehe 24 Novemba 2022, natengua uteuzi wa Mohamed Habibu Mnyaa nafasi ya Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge na Sera.Uteuzi wa kujaza nafasi hiyo utafanyika baadaye na kuwasilishwa katika Kikao kijacho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.”

error: Content is protected !!