Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Asad: Katiba mpya muhimu, nchi imefunguka
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Asad: Katiba mpya muhimu, nchi imefunguka

Spread the love

ALIYEKUWA Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini-CAG, Profesa Mussa Assad amesema licha ya kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Katiba mpya vivyo hivyo kuna umuhimu wa kupatikana viongozi bora watakaoweza kuisimamia katiba hiyo. Anaripoti Faki Ubwa, Dar es Salaam …  (endelea).

Prof. Asad ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Mei 2022 jijini Dar es Salaam baada ya kuwasilisha maoni na mapendekezo yake kwa wajumbe wa Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika maoni yake amependekeza mambo mbalimbali kuhusu suala la utawala bora au viongozi bora wa kuisimamia hiyo Katiba kwani ndilo tatizo kubwa lililopo nchini.

“Ndio maana katika miaka iliyopita tulifika mahala wote tukawa tunaogopa kusema chochote kwa sababu kulikuwa na mtu pale juu ambaye hapakuwa na mtu yoyote aliyelkuwa akimsikiliza,” amesema.

Ameongeza kuwa ni Katiba mpya iweke kipengele kitakachomlazimisha mtu kuchukuliwa hatua iwapo akiivunja.

“Hilo lifanyiwe kazi ili kuhakikisha kwamba mtu akiivunja katiba zipo namna za kumchukulia hatua ili akitokea mtu akavunja katiba ambayo aliiapa aondoke madarakani,” amesema.

Amesema ili kuzingatia misingi ya utawala bora ni muhimu kuwe na mambo matatu ambayo kwanza kuwe na muundo, pili nafasi na tatu watu wa kujaza hizo nafasi.

Amesema mambo yote matatu ni muhimu kwa sababu siku hizi wamekuwa waongo waongo hasa kwa kulemazwa na matumizi ya simu ambayo yamechangia kuongezeka kwa udanganyifu kiasi cha kuwafanya watoto kuhisi uongo ni jambo la kawaida.

“Mwisho tupeane nafasi kwa sababu tunafaa kupewa nafasi si kwa sababu unamjua fulani,” amesema

Alipoulizwa kuhusu tume huru ya uchaguzi amesema kuwa hilo suala muhimu na kwamba kwenye tume zijazwe kisheria.

“Tukubaliane sote nani anastahili kukaa kwenye ile nafasi kwa elimu na kwa uzoefu wake sio mtu atoke chuo kikuu kwa sababu alikuwa Daktari basi awe mjumbe wa tume ya uchaguzi.

“Lazima awe amehudumu nafasi fulani kwa muda fulani, sisi wenyewe tuseme anastahili kwa sababu tumemuona miaka 10 iliyopita sio mtu muongo muongo hana mambo ya ajabu ajabu lakini tukiwa na watu kama wale waliokuwepo inakuwa shida kidogo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amesema hali ya kisiasa sasa nchini imtulia na wawekezaji wamerejea kwa sababu biashara zinafunguliwa na watu wanapewa vibali vya kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!