Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Halanga apongeza vijana JKT kurejeshwa kambini
Habari za Siasa

Mbunge Halanga apongeza vijana JKT kurejeshwa kambini

Spread the love

 

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Asia Halanga amempongeza Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo kwa kuridhia kuwarejesha kambini vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Vijana hao 853 walifukuzwa kambini tarehe 12 Aprili 2021 kutokana na makosa ya kinidhamu lakini 5 Machi 2022, Jenerali Mabeyo aliamuru vijana hao wote kurejea kambini mara moja.

Leo Alhamisi, tarehe 19 Mei 2022, akichangia Bajeti ya Ulinzi na JKT kwa mwaka 2022/23 bungeni jijini Dodoma, Aisia amewapongeza Rais Samian a Jenerali Mabeyo, “namna walivyowaelea na kuwachukulia vijana wale waliofukuzwa kambini na leo wamerejeshwa, nawashukuru sana na kuwapongeza.”

Katika mchango wake, Asia ameiomba Serikali kupitia wizara hiyo kuwafikiria vijana wa JKT waliofanya kazi maeneo mbalimbali kisha kurejeshwa nyumbani kuona namna ya kuwasaidia.

“…ni kweli walifanya kazi kubwa sana ya ujenzi wa miradi mbalimbali. Nina ombi kwa waziri, kuna vijana walitumika kambi ya Ukonga wao walitumika kabla ya wale waliokwenda kujenga ukuta wa Mirerani na Ikulu wao walitumika kujenga Bwawa la Umeme Rufiji, Chuo cha Vetas Lindi., Chuo cha Ualimu Kigoma, Bandari Kavu kwawa, Majengo Mapya, Ofisi ya Manispaa Kinondono.”

“Lakini baada ya kazi kubwa hiyo, vijana wale walichukuliwa na kupelekwa Mgulani na baada ya hapo wakatawanishwa kurudishwa nyumbani na sasa wapo tu wamekaa na tunaiomba sasa serikali iweze kuwafikiria vijana wale kwa jicho la pili,” amesema Halanga

Aidha, mbunge huyo amesema, JKT inafanya kazi kubwa kuwapa ujuzi mbalimbali ukiwemo wa kilimo, “niwaombe vijana inaowapatia mafunzo na kwa sababu wanaujuzi, serikali iweke mkono hapa ofisi ya waziri mkuu ina mikopo mbalimbali ione jinsi ya kuweza kuwasaidia wanapomaliza mafunzo waone jinsi ya kwenda kujiajiri.”

Akihitimisha mchango wake, ameiomba Serikali kwa maana ya Wizara ya Ulinzi kushirikiana na Wizara ya Kilimo na ile ya Viwanda na Biashara kuona jinsi ya kuwasaidia vijana nao wanaopata ujuzi wa kulimo kuweza kuendeleza ujenzi wao baada ya mafunzo.

“JKT inafanya kazi kubwa kuandaa vijana, iangalie jinsi ya kuunganisha nguvu na wizara ya kilimo kwa sababu wizara ya kilimo inatoa fursa kwa vijana, lakini wizara ya viwanda na biashara ili kuwatafutia fursa za masoko, lengo ni kuwakomboa vijana,” amesema

Akijibu baadhi ya hoja za Halanga, Waziri wa Ulinzi, Dk. Stergomena Tax amesema lengo la mafunzo siyo kuwaajiri baada ya kuhitimu bali ni kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kwenda kujiajiri.

“Wanajengewa stadi na kwenda kujitegemea, si rahisi kuwachukua vijana wote kwani lengo ni kuwajengea uwezo,” amesema Dk. Tax

Aidha, amesema amekwisha kuanza mazungumzi na wizara ya kilimo kuona jinsi ya “kuunganisha nguvu kama wizara ya kilimo na ile ya viwanda ili kuona baada ya hapo tunakwenda kuifanya. Tunalifanyia kazi na nimekwisha kuzungumza na waziri wa kilimo ili kuona jinsi ya kuwatumia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!