Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari Mauya miwili tena Yanga
HabariMichezo

Mauya miwili tena Yanga

Spread the love

 

KIUNGO mkabaji wa klabu ya Yanga Zawadi Mauya ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Yanga utakaomfanya kusalia ndani ya kikosi hiko hadi 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezaji huyo ameongezewa mkataba huo hii leo tarehe 19 Mei 2022, jijini Dar es Salaam ambapo ndio makao makuuu ya klabu hiyo.

Mauya ameongezewa mkabata huo ikiwa siku chache, mara baada ya kuifu gia timu yao bao la pili kwa shuti la mbali kwenye mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji.

Huyo anakuwa mchezaji watatu kuongezewa mkataba ndani ya klabu hiyo, katika siku za hivi karibuni kuelekea msimu mpya wa mashindano 2022/23 kwa ajili ya kuboresha kikosi chao.

Mchezaji huyo anaungana na nahodha mkuu wa kikosi hiko Bakari Nondo Mwamnyeto pamoja na Kibwana Shomari ambao wote hivi karibuni wameongeza mikataba ya miaka miwili kuendelea kukipiga ndani ya kikosi hiko.

Mauya alijiunga Yanga kwenye msimu wa 2020/21, akitokea kwenye kikosi cha kagera Sugar ambapo alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu kiasi cha kuwavutia mabingwa hao wa kihistoria nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!