May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wamsaka Kigogo

Spread the love

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Dar es Salaam linamsaka mwanaharakati anayejiita jina la Kigogo katika mtandao wa Twitter. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

‘Mwanaharakati’ huyo anadaiwa kuzusha hofu baada ya kusambaza taarifa za uongo, kwamba Rais John Magufuli anaumwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Ramadhani Kingai, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni leo Jumamosi tarehe 13 Machi 2021, wakati akizungumza na vyombo vya habari mkoani Dar es Salaam.

Kamanda Kingai amesema, jeshi hilo linaendelea kumfuatilia Kigogo, na kwamba wakati wowote litamkamata kujibu tuhuma zinazomkabili za kumzushia ugonjwa Rais Magufuli.

“Bado tunaendelea kufuatilia taarifa za wengine ambao wanasambaza taarifa za kizushi, yeyote atakayesambaza tunapekua kila sehemu, tutazifanyia kazi kuhakikisha wanaohusika wanachukuliwa hatua za kisheria.

“Huyu anayeitwa  Kigogo ni mhalifu kama wengine, tunaendelea kupekua kuhakikisha na yeye tunamtia mbaroni. Muda, siku haijafahamika ila tutamkamata tu,” ameahidi Kamanda Kingai.

https://youtu.be/mBVeOedmFCc

 

Taarifa zinazodai Rais Magufuli mgonjwa, zilianza kusambazwa mitandaoni hasa twitter mapema wiki hii.

Hata hivyo, jana tarehe 12 Machi 2021 akiwa mkoani Njombe, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikanusha madai hayo.

Alisema, Rais Magufuli yupo buheri wa afya na haonekani hadharani kwa sababu, anatekeleza majukumu yake.

error: Content is protected !!