March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi, Dawasco, Tanesco kuanzisha msako mkali

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Tanesco, Dawasco na kampuni mbalimbali za simu za mkononi limeanzisha msako dhidi ya watu wanaohujumu miundombinu ya mashirika hayo. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuanzia tarehe 27 Agosti mwaka huu, litafanya operesheni hiyo kali itaanza kuhakikisha mtandao wa wizi huo unaisha.

“Kumekuwa na wimbi kubwa la watu kujiunganishia maji safi kutoka kwenye mabomba ya DAWASCO bila kufuata utaratibu, pia wanaojiunganishia umeme kinyume na utaratibu, kuiba mafuta ya transformer na kuiba betri kwenye minara ya kampuni za simu hapa jijini Dar es Salaam,” amesema.

Aidha Mambosasa amesema Jeshi la Polisi kuanzia sasa linawataka watu wote wanaojihusisha na uhalifu huo kuacha mara moja  na kujisalimisha wenyewe  katika vituo vya Polisi au katika mashirika na kampuni hizo kabla ya kuanza kwa oparesheni hiyo kali, na watakaokaidi agizo hili watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

error: Content is protected !!