March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

DPP aendelea kuwasotesha Aveva na Kaburu

Spread the love

RAIS wa klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ wameendelea tena kusota mahakamani baada ya kusubiri kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP, kukamilisha hati mpya ya mashtaka na maelezo ya awali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Wakili wa upande wa Serikali Kishenyi Mutalemwa amesema mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo ilipangwa tarehe ya leo kwa ajili ya washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali lakini haitoweza kusoma kwa sababu hati ya mashtaka haijakamilika lakini pia Hakimu mkazi Thomas Simba aliyekuwa anaishikilia kesi hiyo hayupo.

Ikumbukwe hapo awali Hakimu Simba alitaka upande wa mashtaka kubadilisha haraka hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa wawili katika shauli hilo Zacharia Hans Pop na Franklin Lauwo ambao hawakuwahi kufika mahakamani hata siku moja.

Kesi hiyo ambayo imeahilishwa hadi 31 Agosti kwa ajiri ya washtakiwa hao kuanza kusomewa maelezo ya awali baada ya hati mpya ya mashtaka kukamilika.

error: Content is protected !!