February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Okwi kuikabili Taifa Stars Septemba

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda ‘The Crains’ kitakachowakabili timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ mchezo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Mataifa Afrika, utakaochezwa tarehe 8 Septemba, mwaka huu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Okwi ambaye alikuwa katika kiwango kizuri katika msimu uliomalizika baada ya kupachika mabao 20 na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara na ndani ya klabu yake ya Simba.

Mbali na mshambuliaji huyo Kocha mkuu wa The Cranes, Sebastien Desabre amemjumuisha beki wa kati wa klabu ya Simba, Juko Murushid katika orodha ya wachezaji 30 watakaomenyana na Taifa Stars kwenye Uwanja wa Mandela, Nambole nchini Uganda.

Wengine walioitwa katika kikosi hicho ni Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Jamal Salim (El Meriekh), Charles Lukwago (KCCA FC) and Nicholas Sebwato (Onduparaka FC), Isaac Isinde (Kirinya Jinja SS), Murushid Juuko (Simba SC), Timothy Awanyi (KCCA FC), Denis Iguma (Kazma FC), Nicholas Wadada (Azam FC), Musitafa Mujuzi (Proline FC).

Godfrey Walusimbi (Gor Mahia) FC, Isaac Muleme (Haras El Hodood), Joseph Ochaya (Lusaka Dynamo), Hassan Wasswa (El Geish), Khalid Aucho(Un attached), Ibrahim Saddam Juma (KCCA FC), Tadeo Lwanga (Vipers SC), Opondo Moses( Vendsyssel)

Allan Kateregga (Cape Town City), Faruku Miya (Gorica ), Moses Waisswa (Vipers Sc), Yunus Sentamu (FK Tirana), Martin Kizza (Sc Villa Jogoo), Allan Kyambadde (KCCA FC), Emma Okwi (Simba SC), Edrisa Lubega (SV Ried), Derrick Nsibambi (Smouha), Patrick Kaddu (KCCA FC), William Luwagga Kizito (FC Bate Borisov), Yasser Mugerwa (Fasil Kenema).

error: Content is protected !!