Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara NMB yatoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara Dar
BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yatoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara Dar

Spread the love

BENKI ya NMB kupitia Klabu za Biashara ‘NMB Business Club’ imeandaa mafunzo ya kifedha kwa wafanyabiashara jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa benki hiyo wa kuongeza ushirikishwaji wa kifedha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

NMB Business Club ni jukwaa la benki ya NMB linalolenga wateja wadogo na wa kati (MSME) na linawapa wafanyabiashara fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo ya biashara, mbinu bora za soko na huwawezesha kupata mafunzo kuhusu mada mbalimbali za biashara.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Karolina Mthapula (kulia) akipokea tisheti kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini, Ladislaus Baraka (kushoto). Tisheti zitakazovaliwa na katika maadhimisho ya Kilele cha mbio za mwenge nchini ni miongoni mwa udhamini wa shilingi milioni 62 wa Benki ya NMB katika kufanikisha shuguli hiyo pamoja na maonesho ya wiki ya Vijana kitaifa, shuguli ambazo zote zinafanyika Babati, Mkoani Manyara.

Mafunzo hayo yalijumuisha moduli mbalimbali za biashara ikiwa ni pamoja na ufadhili endelevu, uchambuzi wa gharama, uandaji wa bajeti na utunzaji wa kumbukumbu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja yaliyowakutanisha mamia ya wafanyabiashara Jijini Dar es Salaam tarehe 9 Oktoba 2023, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper alisema benki yake imejipanga kuendelea kutoa elimu ya kifedha kwa wateja wake ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi.

“Elimu ya kifedha ni kipaumbele kwa Benki ya NMB. Tayari tumetoa mafunzo mbalimbali ya kifedha kote nchini mwaka huu kama sehemu ya utekelezaji wa dhamira yetu ya kuimarisha ujumuishaji wa kifedha. Elimu ya kifedha imekuwa jambo la lazima kwa kila mtu hasa kwa wafanyabiashara ndiyo maana tunajitahidi kila mara kama benki kuiboresha,” alisema.

Prosper alisema benki yake ya NMB itaendelea kutumia wataalam kutoa elimu ya masuala ya kifedha ili kuwawezesha wateja wake kufanya vizuri huku akibainisha kuwa benki yake vilevile hutumia fursa hiyo kusikia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.

“Majukwaa ya mafunzo ya Klabu za Biashara ya NMB sio tu kwamba yanatoa ujuzi wa kifedha lakini hutuwezesha kupata maoni ya wateja na kuongeza uhusiano na wateja wetu wa biashara,” alisema

Prosper wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutoa suluhu za kibenki kwa wateja wake na kuwataka wafanyabiashara kuchangamkia suluhu za malipo za kidijitali za benki hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa NMB Business Club Kanda ya Dar es Slaam Award pandilah wakati wa hafla hiyo aliipongeza benki hiyo kwa kujitolea kusaidia ukuaji wa wafanyabiashara kote nchini huku akisema kuwa benki hiyo imekuwa chachu ya biashara nyingi nchini.

Hata hivyo aliitaka benki hiyo kuzingatia kupunguza riba za mikopo ili kuwawezesha wafanyabiashara wengi  kuchukua mikopo yakuendeleza biashara zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!