Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yakabidhi hundi ya Sh milioni 10 kwa Chaneta
Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi hundi ya Sh milioni 10 kwa Chaneta

Spread the love

BENKI ya NMB imekabidhi Sh.10 milioni kwa Chama Cha Netiboli Tanzania (CHANETA) ikiwa na udamini wa Club Bingwa wa Netiboli Ligi Daraja la Kwanza ambayo inafugiliwa leo Ijumaa tarehe 8 Julai 2022 Uwanja Taifa wa Benjamin Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yatakutanisha timu 29 za netiboli kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya udhamini kwa Chama cha Netibilo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alisema udhamini huo unaendana na mkakati wa benki hiyo wa uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaosaidia sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya na michezo miongoni mwa sekta yingine.

“Leo tunakabidhi hundi ya million 10 ikiwa ni udhamini wetu kwa Ligi Daraja la Kwanza,” alisema.

“Udhamini huu kama sehemu ya juhudi zetu za kusaidia maendeleo ya shughuli mbalimbali za michezo. Kama benki, tumekuwa na mchango mkubwa katika kufadhili michezo mbali  mbali katika uwanja wa mpira wa miguu na gofu miongoni mwa michezo mingi,” alisema.

Richard wakati wa hafla hiyo alisisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya michezo na kuongeza kuwa benki inaelewa kuwa michezo leo imegeuka kutoka kwa njia ya mazoezi ya mwili na kuwa njia ya ajira.

“Kama benki, tunatambua kuwa michezo ni fursa ya ajira hasa kwa vijana katika dunia ya sasa. Kwa kutambua hilo benki yetu itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ya michezo ili kujenga miundombinu muhimu na kuhakikisha kunakuwa na mazingira bora ya michezo,” alisema.

Awali, Mwenyekiti wa CHANETA, Devotha John alibainisha kuwa mashindano hayo ni sehemu ya mkakati wa maendeleo wa chama cha miaka mitano unaolenga kufufua mpira wa wavu kuanzia ngazi ya chini.

“Mashindano haya ni ya kihistoria kwani yatakutanisha pamoja idadi kubwa ya timu katika historia ya netiboli nchini,” alisema.

Aliongeza kuwa pamoja na kukuza vipaji vipya, mashindano hayo ni jukwaa la kutafuta wachezaji wa timu ya netiboli ya Twiga Queens.

“Tutatumia ligi hii kama jukwa la lutafuta vipaji vipya vya timu yetu ya taifa ya netiboli Taifa Queens. Tunaamini wachezaji watakaotambulika wataisaidia timu katika michuano ijayo ya kikanda na kimataifa,” alisema.

Mashindano hayo yanaanza leo na yanatarajiwa kumalizika Julai 19, 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!