Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB, Simba SC. waja na ‘Ukaribu wa Nguvu’ kusajili wanachama, jezi kuzinduliwa kileleni mwa Kilimanjaro
BiasharaMichezo

NMB, Simba SC. waja na ‘Ukaribu wa Nguvu’ kusajili wanachama, jezi kuzinduliwa kileleni mwa Kilimanjaro

Spread the love

BENKI ya NMB na Klabu ya Simba, zimezindua ushirikiano wa kibiashara uliopewa jina la ‘Ukaribu wa Nguvu,’ kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kufanya usajili wa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumzia ushirikiano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC., Imani Kajula, amesisitiza kuwa Ukaribu wa Nguvu unalenga pia kuwafanya wadau wa Simba washabikie timu yao kwa faida.

Ukaribu wa Nguvu ni mwamvuli unaojumuisha akaunti tatu za NMB Simba Account, NMB Simba Queens Account (Malkia – kwa wanawake) na NMB Simba Mtoto Account (kwa watoto).

Amesema mashabiki na wanachama wa Simba watajisajili kupitia mtandao mpana wa matawi 229 ya Benki hiyo, ambako watapewa kadi zenye Bima ya Maisha ya hadi Sh. Mil. 6.

Uzinduzi hu umefanyika Jumamosi hii kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam, ambalo mbali na Kajula, Simba iliwakilishwa pia na Mwenyekiti wake Murtaza Mangungu.

NMB iliwakilishwa na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, Afisa Mkuu wa Biashara ya Kadi, Philbert Casmir na Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi, Donatus Richard.

Akizungumza katika uzinduzi huo mbele ya mamia ya mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba, Mponzi alisema ushirikiano huo baina ya taasisi hizo kubwa nchini, unaenda kunufaisha pande zote.

Alisema wana Simba watafaidika zaidi kwani watahudumiwa na benki yake hiyo kupitia bidhaa zao, ikiwemo ya Mshiko Fasta – mikopo nafuu isiyo na masharti inayoanzia Sh. 1,000 hadi 500,000 kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo.

“Tuna mtandao mpana wa matawi, ambao tunaenda kuutumia kuwafikia Watanzania wote wanaoipenda Simba, ambao watapata kadi za NMB zenye logo ya Simba, ambazo watazitumia Kufanya miamala, sambamba na ofa za mapunguzo ya asilimia 10 na kuendelea watapolipia huduma kupitia kadi zao hizo.

“Mashabiki wajitokeze matawini kote nchini kuanzia leo kufungua akaunti zao na wale waliokuwa na akaunti za NMB hapo kabla, watabadilishiwa kadi zao na kupewa mpya zenye logo ya klabu yao pendwa.

“Tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha mchakato huu, pamoja sajili za Wana Simba wote katika Wiki ya Simba (Simba Week) inayoanzia Agosti 1,” alibainisha Mponzi na kuongeza ya kwamba makubaliano baina ya NMB na Simba yaneanda kuwapa faida kubwa mashabiki wa klabu hiyo aliyoipongeza kwa kushika nafasi ya Saba ya ubora Afrika.

Kwa upande kwake, Kajula alisema: “Mashabiki Simba wanapaswa kuwa ushabiki wa faida, ndiyo maana wamekuja na akaunti na kadi hizo ambazo Mwanasimba atafungua akaunti kwa Sh. 5,000 na akaunti zote zitaambatana na bima za maisha.

“Tumeingia nao mkataba, NMB kwa kuwa wana mawakala na matawi mengi nchini, wana zaidi ya mawakala elfu 20 nchini,” alisema Kajula.

Naye Mangungu alisema: “Tumeingia mkataba wa ushirikiano na NMB ambapo ushirikiano huu kwa kiasi kikubwa ndiyo unatusaidia kuendesha timu, kusajili wachezaji wazuri na mengineyo.

“Kwa mashabiki wetu ambao walikuwa na kadi na taasisi nyingine ambazo tulikuwa tunashirikiana nazo huko nyuma tunawaomba wahamie NMB sasa,” alisema.

Ikumbukwe kuwa Simba inakuwa klabu ya pili NMB kuingia nayo mkataba wa kutoa kadi za mashabiki baada ya hivi karibuni kuingia mkataba kama huo na mabingwa wa kihistoria wa soka la Tanzania, Yanga.

Katika hafla hiyo, Simba walimtambulisha winga wao mpya Mcameroon, Willy Essomba Onana aliyetua Msimbazi akitokea Rayon Sports ya Rwanda, ambapo pia walitangaza tarehe za uzinduzi wa jezi mpya kuwa Julai 21 kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, pamoja na siku ya Tamasha la Simba Day, Agosti 6.

Kajula alitangaza kuwa jezi mpya za Simba SC za msimu wa 2023/24 zitazinduliwa rasmi tarehe 22 Katika kilele cha mlima Kilimanjaro mkoa wa humo.

Jukumu la kupeleka jezi katika kilele cha mlima Kilimanjaro amekabidhiwa meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

error: Content is protected !!