October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NMB kunufaisha sekta ya kilimo Tanzania

Spread the love

BENKI ya NMB imeweka adhma ya kuiboresha sekta ya kilimo nchini Tanzania kwa kutoa suluhisho bora na nafuu kwa shuguli za kilimo na zilizo katika mnyororo huo wa thamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Haya yameelezwa na Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi alipokuwa katika maonesho ya kitaifa ya Nanenane yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Mponzi alisema Benki ya NMB imetumia fursa ya kuwa na banda katika maonesho hayo kutoa Elimu kwa wakulima lakininpia kuwaelezaea fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuwanufaisha na kunufaisha shuguli zao za kilimo, Ufugaji na uvuvi.

Afisa Mkuu wa Biashara na wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Benki ya NMB kwenye maonyesho ya Nanenane jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Biashara wa Benki hya NMB, Isaac Masusu na kulia ni meneja wa benki hiyo wa kanda ya nyanda za juu, Straton Chilongola

“Katika Banda la NMB tumekuwa tukitoa Elimu kwa wakulima zitakazo wasaidia katika shuguli zao, lakini pia elimu ya fedha ambayo ni muhimu sio tu kwa ajili ya kilimo lakini pia kwa mustakabali wa Maisha yao kwa ujumla,” alisema Mponzi.

“Katika sekta ya kilimo, tumekuwa wa kwanza kutoa mikopo yenye riba nafuu zaidi ili kuhakikisha sekta hii inasonga mbele kwani Imani yetu ni kuwa kukuza kilimo ni chachu kubwa sana ya kuukuza uchumi wa nchi yetu,” aliongeza

“Mbali na kiasi cha trillion 1.56 ambazo tayari tumeshatoa katika sekta ya kilimo kwa kipindi cha miaka mitano, tumetenga kiasi cha Bilioni 20 kwaajili ya kujenga maghala yatakayotumika kuhifadhi mazao baada ya kuvuna. Tunatambua Changamoto kubwa ya uhifadhi wa mazao kwa wakulima nchini na tunaamini kiasi hiki kitakwenda kuwa chachu ya uhifadhi wa mazao wenye tija kwa wakulima,” Alisema Mponzi.

Kwa kuonesha umuhimu na thamani kubwa ya sekta ya kilimo nchini na kwa benki ya NMB, benki hii imekuwa ni miongoni mw wasdhamini wakuu wa maonesho ya Nanenane kwa mwaka huu hukju ikitoa udhamnini wa milioni 60.

Afisa mkuu huyo wa benki hiyo NMB ameendelea kuwasisitiza wakulima na watanzania kwa ujumla kuendelea kutumika matawi ya Benki ya NMB kujipatia Bima mbalimbali ambazo zitawafanya kuendeleza kufanya kazi zao kwa kujiamini na kutokuwa na hofu na hivyo kuongeza uzalishaji.

“Kupitia tawi lolote la NMB, unaweza kujiwekea bima za makampuni mbalimbali ya Bima ambayo tunafanya nao kazi kwa Pamoja ili kuweza kuwafanya wateja wetu kuendela kufanya shuguli zao kwa kujiamini kwani endapo itaokea hasara ya namna yeyote basi bima itakuwepo kwaajili ya kuwafidia,” alisema

“Kwa wakulima na wafugaji, zipo bima nzuri kabisa kwaajili yao ambazo zitawasaidia hata katika kipindi ambacho wanakumbana na hasara katika uzalishaji au hata wanapokumbana na majanga mbalimbali. Hivyo kwa kujiwekea Bima, bado wakulima, wafugaji na wavuvi watakuwa na uhakika wa uzalishaji mkubwa,” alisema Mponzi.

Benki ya NMB imeshiriki maonesho ya nanenane ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika kilele chake cha siku ya nanenane.

error: Content is protected !!