Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Niwemugizi: Rais Samia usikubali kulinganishwa na Mungu, ‘kazi yetu kukosoa, kuonya
Habari za SiasaTangulizi

Niwemugizi: Rais Samia usikubali kulinganishwa na Mungu, ‘kazi yetu kukosoa, kuonya

Spread the love

 

ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Rulenge-Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan asikubali kamwe kulinganishwa na Mungu kwa namna au siku yoyote au kuitwa Mtukufu.

Pia amesema viongozi wa dini ni sauti ya Mungu katika jamii kwamba Mungu anasema na watu wake wote kupitia midomo yao hivyo ni wajibu wao kukemea, kuonya pale watu wanapokengeuka na kufundisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kagera  … (endelea).

Askofu Niwemugizi ametoa kauli hiyo leo tarehe 22 Februari, 2022 mjini Ngara mkoani Kagera wakati akitoa salamu za shukrani kwa wageni waliohudhuria sherehe za Jubilee ya miaka yake 25 ya uaskofu wake.

Katika sherehe hizo Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi huku maaskofu mbalimbali wa majimbo yote Tanzania wakihudhuria.

“Rais nikuombea uwe na afya njema na uwe mnyenyekevu lakini pamoja na madaraka makubwa uliyonayo usikubali kamwe kulinganishwa na Mungu namna yoyote ile siku yoyote. Nakumbuka Hayati Mkapa sana alikataa kuitwa mtukufu Rais hili liwe neno kwako.

“Nakuombea Mungu akusaidie kukuza upendo kati ya Watanzania unaotuongoza, ukuze haki nayo haki izae amani na utulivu na kukuza demokrasia katika nchi yetu.

“Ukuze upendo na mshikamano wa watanzania ili hatimaye utumishe wako utukuke na kuacha alama itakayonenwa kwa vizazi vingi, Mungu akujalie hekima na uvumilivu wa kusikiliza hata yale yanayokera masikio yako,” amesema.

Aidha, amesema viongozi wa dini ni watoto wake lakini wengine tuko wakorofi hivyo Mungu amjalie hekima na uvumilivu hasa wanapotoa ushauri.

Askofu Niwemugizi ambaye mwaka 2017 ahojiwa uraia wake na Idara ya Uhamiaji na kuzuiliwa ‘passport’ yake ikiwa ni miezi michache baaba ya kusema ataidai Katiba Mpya hata akiitwa mchochezi, alimuomba Rais Samia awe na hekima kwa kuwa baadhi yao ni wakorofi.

“Unajua sisi watoto wako wengine tuko wakorofu, Mungu akujalie tu hekima na uvumilivu hasa pale unapokuwa ni ushauri wenye nia njema ya kulijenga Taifa letu liendelee kuheshimika ndani na nje ya mipaka yake,” alisema Askofu Niwemugizi jana.

Askofu Niwemugizi ambaye alitawazwa kuwa Askofu mwaka 1997 huku Hayato Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Mkapa wakishuhudia, amesema si kweli kwamba viongozi wa dini ni wanasiasa kwa sababu tu wanapojisemesha – semesha.

“Sisi ni sauti ya Mungu tunatumwa kuwasemea watu wote ni wajibu wetu kuikemea, kuonya pale watu wanapokengeuka na kufundisha watu waishije katika nyanja zote za maisha iwe kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kidini nk.

“Waishi maisha yanayompendeza Mungu, hata wewe ni mtu wangu kukuambia jambo,” amesema.

Mbali na kuutangazia umma kuwa atamuunga mkono Rais Samia na kuendelea kushirikiana na Serikali, pia Askofu Niwemugizi amempongeza kwa kuliongoza Taifa ukitekeleza miradi mingi yenye tija na manufaa makubwa kwa watanzania wote, hongera sana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!