Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Michezo Kibwana, Djuma Shaban tayari kuikabili Mtibwa
Michezo

Kibwana, Djuma Shaban tayari kuikabili Mtibwa

Spread the love

 

WALINZI wa pembeni wa klabu ya Yanga, Djuma Shabani na Kibwana Shomari watakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoshuka dimba ni kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mchezo huo wa kufunga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utapigwa kwenye dimba la Manungu Complex, siku ya Jumatano tarehe 23 Februari mwaka huu majira ya saa 10 jioni.

Akielezea hali ya kikosi chao, msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema kuwa kuna baadhi ya wachezaji wataukosa mchezo huo kufuatia kuuguza majeruhi yao, na kutokuwa sehemu ya mchezo huo.

“Bado kuna wachezaji ni majeruhu, kama Abdalah Shaibu “Ninja” ambaye bado anauguza majeraha yake, Braison David na jesus Moloko nao hawatoweza kucheza mchezo huo.”.

Kwa upande mwengine pia amsemaji wa klabu hiyo aliwazungumzia wachezaji ambao wanarejea dimbani mara baada ya kukosa baadho ya michezo ya nyuma, kwa sababu tofauti tofauti.

“Lakini kuna wachezaji wameshaanza kupona na kufanya mazoezi, Kibwana Shomary tutaenda nae, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amesharejea sambamba na Yassin Mustapha pia na Djuma Shabani ambaye amemaliza adhabu yake.”

Yanga inashuka dimbani dhidi ya mtibwa huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote kwenye Ligi mpaka sasa, mara baada ya kucheza michezo 14 huku wakiwa vinara kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 36, alama tato nyuma ya Simba waliokuwa kwenye nafasi ya pili.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!